Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Rais Magufuli ni mzima na anachapa kazi. Wanataka atoke, atoke aende wapi? Kariakoo au Magomeni?

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Rais Magufuli ni mzima na anachapa kazi. Wanataka atoke, atoke aende wapi? Kariakoo au Magomeni?

Labda ilikuwa ni ule mpango wa kumtuma makamu Tanga asijue jamaa karibu anakata kamba wamuweke ''mtu''wao, kabla General Mabeyo kuutibua.
 
Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, amewataka watanzania wawapuuze Wapotoshaji wa mitandaoni wanaotaka kuleta taharuki juu ya Afya ya Rais Magufuli "Rais ana shughuli nyingi, Wanataka atoke aende wapi, Kariakoo au Magomeni tangu lini?"

Leo asubuhi wakati nakuja huku nimeongea naye kwa simu na ameniagiza niwaambie wana Njombe kuwa anawapenda sana na anawashukuru sana kwa kura nyingi mlizompigia

Kuna wenzetu hawaishi hapa nchini, wao kazi yao ni kutuombea mabaya tu, kupandikiza chuki tu. Sasa unamuombea mwenzako kufa hiyo ni akili kweli? Nawatoa hofu watanzania, Rais wenu yuko imara anafanya kazi zake kama kawaida za ofisini.

Tuhakikishe tunamuabudu Mungu, tunamuomba Mungu katika kila jambo, tunamtegemea Mungu katika kila jambo, hata asubuhi nilivyokuwa natoka Dodoma nimempigia kumjulisha ratiba yangu, hata juzi alikuwa anajua ninakuja akanituma, wasalimie wana Njombe na nilitoa Salamu.

Naomba nirudie, kwa salam alizotupa leo kweli wana Njombe, mheshimiwa Rais anawasalimia sana wana Njombe, mheshimiwa Rais anawashukuru wana Njombe.

Wakati PM Majaliwa amayasema haya,kumbe Mzee wa watu alikuwa tayari amekwisha 。。。!Je, leo inaweza kuwa ndio ile siku? Ukweli halisi ni upi? Nini hasa kilitokea na kwanini tulijulishwa baada ya siku 5?
Aliyenijulisha tarehe hii ni kijana wao mwenyewe na hapa kijana huyo akathibitisha Silent Hero Huyu ni Mzalendo wa Kweli wa Taifa Hili, Ndie Aliyefanya Katiba Ifuatwe Mama Akawa!. Apewe Maua Yake!... Stahiki ni kuwa DGIS in Future!
P
 
Wakati PM Majaliwa amayasema haya,kumbe Mzee wa watu alikuwa tayari amekwisha 。。。!。
P
Kwa maelezo ya rais Samia, alilazwa trh 6, saba akatoka hosp. Kisha trh 14 akazidiwa na kupelekwa hos. Hadi mauti trh 17

Kumbe nyie wazee wa bawa la tai mlikuwa mnajua kila kitu afu mkaacha sisi tunadanganywa?
 
Mjomba wangu ni afisa kipenyo mwandamizi kuna jambo zito kaniambia.

Waziri mkuu kama anabisha amwambie Magufuli anyooshe kidole juu ama afanye kama anajikuna halafu apigwe picha.
Hii comment yako siku tano baadae ndio umma ukatangaziwa...aiseee
 
Kwa maelezo ya rais Samia, alilazwa trh 6, saba akatoka hosp. Kisha trh 14 akazidiwa na kupelekwa hos. Hadi mauti trh 17
Sa100 mwenyewe alidanganywa!
Kumbe nyie wazee wa bawa la tai mlikuwa mnajua kila kitu afu mkaacha sisi tunadanganywa?
kijana wao ndio aliirusha youtube usikuwa saa 7 usiku !。haikuwahi kukanushwa na hapa ameeleza mwenyewe Silent Hero Huyu ni Mzalendo wa Kweli wa Taifa Hili, Ndie Aliyefanya Katiba Ifuatwe Mama Akawa!. Apewe Maua Yake!... Stahiki ni kuwa DGIS in Future!
P
 
Rais John Joseph Pombe Magufuli piga kazi kuwaletea na kuwajengea misingi imara ya kimaendeleo Watanzania nilichogundua Watanzania wanampenda sana Rais wao kiasi cha kutokumuona wala kumsikia ndani ya wiki kila mmoja amekuwa hana raha kwa kuwa wameshazoea kumsikia akiwapa maagizo wateule wake na kutatua kero za wananchi.

Kwa dalili hizi ni kipimo cha mapenzi kilichopitiliza najua wenye account fake wakiwa peke yao au kwenye vikao vyao wanazungumzia muziki mnene wa mtetezi wa wanyonge.

Tuendelee kumuombea kwa Mungu raisi wetu azidi kuwa na afya njema na amuepushe na wenye husuda na roho mbaya ili aweze kutekeleza yale yote aliyo ahidi kipindi cha kampeni kupitia ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Raisi wetu wananchi wamekumiss na wanakupenda sana muda utakaonekana ama hakika watashangilia kama kumefungwa goli uwanja wa taifa!

Hapa kazi tu, tusisahau kufuata muongozo wa wataalamu wa afya Covid19 ipo!
Ameen
 
Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, amewataka watanzania wawapuuze Wapotoshaji wa mitandaoni wanaotaka kuleta taharuki juu ya Afya ya Rais Magufuli "Rais ana shughuli nyingi, Wanataka atoke aende wapi, Kariakoo au Magomeni tangu lini?"

Leo asubuhi wakati nakuja huku nimeongea naye kwa simu na ameniagiza niwaambie wana Njombe kuwa anawapenda sana na anawashukuru sana kwa kura nyingi mlizompigia

Kuna wenzetu hawaishi hapa nchini, wao kazi yao ni kutuombea mabaya tu, kupandikiza chuki tu. Sasa unamuombea mwenzako kufa hiyo ni akili kweli? Nawatoa hofu watanzania, Rais wenu yuko imara anafanya kazi zake kama kawaida za ofisini.

Tuhakikishe tunamuabudu Mungu, tunamuomba Mungu katika kila jambo, tunamtegemea Mungu katika kila jambo, hata asubuhi nilivyokuwa natoka Dodoma nimempigia kumjulisha ratiba yangu, hata juzi alikuwa anajua ninakuja akanituma, wasalimie wana Njombe na nilitoa Salamu.

Naomba nirudie, kwa salam alizotupa leo kweli wana Njombe, mheshimiwa Rais anawasalimia sana wana Njombe, mheshimiwa Rais anawashukuru wana Njombe.

Uzi unatimiza miaka minne kesho🤣🤣
 
Back
Top Bottom