View attachment 2390917
MIWA YA KIKUNDI CHETU IMECHOMWA MOTO KABLA YA MUDA WA KUVUMWA NAKUTUSABISHIA HASARA YA MAMILIONI YA SHILINGI.
Huyu ni mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wilaya ya Kilosa. Ukweli ni kwamba yupo hapo kwenye uongozi siyo kwa nia ya kusaidia wananchi anaowaongoza bali ni kwa ajili ya kujilinda na kujinufaisha kwa kutumia nyazifa aliyonayo.
Ameweza kununua shamba lenye thamani ya shilingi BILIONI MOJA kwa shilingi MILIONI MIA TATU TU.
JINSI ILIVYOKUWA.
Shamba hili lenye ukubwa wa ekari 499 Namba M19 lililopo Mbigiri-Kilosa lilikuwa linamilikiwa na mtu anayeitwa Pascal Mbwete. Kikundi cha wananchi wanajihusisha na kilimo cha miwa, walikodisha shamba hili ili walime miwa ya sukari.
Kupitia chama chao kikuu cha ushirika walifanikiwa kupata mkopo kutoka benki ya Azania. Baada ya kupewa mkopo wenye thamani ya shilingi milioni 578, waliandaa shamba ambalo lilikuwa pori, wakaweka miundombinu ya visima na kununua magenereta pamoja na simtank kwa ajili ya kujazia maji ya kumwagilia miwa.
Baada ya hayo kufanyika, ilikuja taarifa kuwa Yule mmiliki wa shamba anadaiwa na Benki ya watu wa India shilingi bilioni moja na Benki inatangaza kulipiga mnada shamba hilo kwa shilingi Bilioni moja.
KIkundi kiliwasiliana na mmiliki wa shamba kutaka kufahamu ukweli wa madai hayo ya Benki, naye alikiri kudaiwa kiasi hicho cha pesa. Alieleza alichukua mkopo kwa ajili ya kujishughulisha na biashara lakini biashara zake zilipata changamoto na kupata hasara.
Kikundi kilijaribu kuwasiliana na Benki ya Watu wa India ili walilipe deni hilo kwa awamu(installments) punde watakapofanikiwa kuvuna miwa na kuiuza.
Kabla ya kupata mawasiliana na maelewano na Uongozi wa Benki ya Watu wa India, alitokea huyu mwenyekiti wa CCM wilaya na kulinunua shamba hilo kwa shilingi milioni mia tatu tu.
WANAKIKUNDI TUNASHANGAZWA NA MAMBO YAFUATAYO;
- Inakuwaje kwa kiongozi ambaye anapaswa kutusaidia sisi wanakikundi wa hali ya chini kupambana na kulipa deni hili badala yake anapambana na sisi kulichukua shamba hili kwa manufaa yake binafsi?
- Kiongozi ni mtu wa kusaidia anaowaongoza au ni mtu wa kuwakandamiza?
- Inakuwaje shamba lenye thamani ya shilingi BILIONI MOJA, yeye amelinunua kwa MILIONI MIA TATU TU!?
HATUA TULIZOCHUKUA WANAKIKUNDI MPAKA SASA.
Wanakikundi tumejaribu kuomba msaada kwa viongozi mbalimbali ikiwemo ofisi ya mkuu wa mkoa, lakini majibu tunayopewa ni “TUSUBIRI SUALA LETU LINASHUGHULIKIWA”. Imeshapita miaka zaidi ya mitatu sasa bado tunaambiwa tusubiri.
UKWELI KUHUSU KIGOGO HUYU WA CHAMA.
Ukweli ni kwamba mwenyekiti huyu wa chama tawala anatumia cheo chake na uwezo wake kifedha kufanya “robbin” kwenye ngazi mbalimbali za uongozi. Viongozi karibu wote amewaweka “mfukoni”, kuanzia ngazi ya kata hadi mkoa hakuna anayeweza kumtisha.
MADHIRA TUNAYOYAPATA WANAKIKUNDI.
- Tumezuiliwa kufanya shughuli yoyote ya kilimo kwenye shamba hilo. Miundombinu yetu tuliyoweka inaharibiwa na miwa iliyomichanga kuchomwa moto.
- Hakuna kiongozi wa kutusaidia kwani wengi wanamuhofia huyu mwenyekiti atawakata majina yao punde watakapoamua kugombea uongozi wa chama.
- Viongozi wetu wanafunguliwa kesi za kuundwa ili kuwadhoofisha.
- Miwa yetu imechomwa moto kabla ya muda wa kuvumwa, tumeripoti polisi, tukamleta afisa kilimo kufanya tathimini akasema miwa haina thamani yoyote.
Inasemekana kuwa miongoni mwa viongozi wa kikundi chetu walipingana na huyu “mwamba” kwa kutompigia kampeni kwenye mambo ya uongozi. Kwahiyo anafanya hivi kwa lengo la kumkomoa, lakini kiualisia tunaumia sisi ambao hayo mambo ya uchaguzi hayatuhusu.
Tabia hii ya kuwaonea wananchi wa maisha ya chini kwa kupora mashamba yao si ngeni kwake. Alishawai fanya hivi mara kadhaa na waziri mkuu Kassim Majaliwa alifika Kilosa na kuamuru arudishe mashamba ya hao wananchi.
MAOMBI YETU KWA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA.
Tunakuomba ulione hili jambo na kutusaidia ili tuweze kurejea kwenye shamba letu na kuendelea na kilimo kwani tunamkopo wa shilingi milioni mia tano na themanini(580mil) kwenye benki ya Azania. Ili tuulipe tunaitaji kulima miwa na ili tulime miwa tunaitaji shamsba hili ambalo tayari kuna miundombinu yetu.
Sisi kama wanakikundi tulikuwa tayari kulipa deni la Benki ya Watu wa India kwa awamu punde tutakapovuna miwa yetu.
TUNAAMINI WEWE WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA JAMBO HILI UTALIPATIA UFUMBUZI.
Regards;
Mwanakikundi mnyanyasika.