Waziri Mkuu Kassim Majaliwa tusaidie huyu kigogo wa CCM Kilosa anatuonea wananchi

Hayo ni Majungu nilichokielewa kuwa huyo jamaa amelinunua hilo shamba na kama hicho kikundi lingekuwa serious wangelitwa kwa kulinunua.hapo hakuna unyanyasaji na kama ni wa CCM kwani yy hana haki?Au haki yake imetwaliwa kwa kuwa ni mwanakijani?
Nafikiri haujakielewa nilichoandika.
Hakuna majungu hapo...labda maana ya neno "jungu" ipo zaidi ya moja.
 
😁😁😁 me nawaombea dua njema . mkuu asikilize malalamiko yenu lakini mmmh 😁😁😁 nchi ngumu hii
Thank u.
Ni kweli nchi ngumu ila hakuna namna tutaishi tu kwani kwenda Burundi si rahisi.
 
Siyo kila kitu kinaweza amuliwa na sheria mkuu........kuna kitu kinaitwa maamuzi ya busara na hekima.
Tatizo kubwa ni watanzania kufikiri sheria ni ya watu fulani tu.
Sheria inamlinda kila mtu na inaweza kulinda haki ya mtu yeote, itumie vizuri tu.
 
Mkuu nilichokiandika kinaeleweka........no need to mention a name.
 
Magufuli alimchana live hadharani nadhani anamfahamu vizuri
 
Mkuu umeandika kitu fulani..........
Anyway, thank u.
 
Baadaye mtavishwa kanga za kijani mtatamba mtaani tieni kwa roho moja!! Tulieni tuli dawa iwaingie!!
Mkuu kikundi hiki hakina chama....kila member ana chama chake cha siasa.
Si rahisi kwa ulichokiandika.
Anyway, thank u.
 
Nilivyoelewa mimi hapo huyo mwenyekiti hana makosa,shamba ni lake hivyo ana haki ya kufanya anachotaka.
hata kama kanunua milion 300 kama unavyosema, hiyo benki inayoliuza si ilikubali kuuza?? Inaonekana huyo mmiliki aliyechukulia mkopo bila kuwashirikisha katika hilo ndio mwenye makosa.
sioni makosa ya huyo mwenyekiti na nadhani hata mkienda mahakamani mtapigwa chini.

hoja ya mwenyekiti wa ccm, kunyimwa kampeni, kusema huyo jamaa ni mnyanyasaji na kukimbilia huku jf badala ya kwenye mamlaka zinaonesha kitu fulani kuhusu wewe.
 
Magufuli alimchana live hadharani nadhani anamfahamu vizuri
Ni kweli ...alimwambia ukweli wake. Baadaye Majaliwa alikuja kumpokonya kile aliwachulia wananchi.
Shida ya viongozi wetu hawa wanataka kila sehem ya Tanzania hii apate eneo kubwa kwa kutumia uongozi wake.
 
Mwanzoni si ulisema myie mi wakodishaji? sasa unasema shamba lenu, kwanini mnapenda short cut? Nna wasiwasi nyie ndio wadhulumaji mnataka mumtumie Waziri Mkuu kunyanganya haki ya mtu. Huyo mwenyekiti si amenunua kwa mwenye shamba? Sasa we mkodishaji inatokeaje unathaminisha mali ya mtu mwingine? Mwenye shamba ameuza kwa sh. 300M we unasema thamani yake ni Bilioni moja. Who are you? We ni mkodishaji tu.
 
Ulichokiandika unaweza ukawa sahihi kwa upande fulani...lakini ukisoma critically utaona wapi kuna shida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…