Nchi yetu siyo kisiwa, Hivyo Ni lazima ishirikiane na nchi nyingine kidiplomasia na Ni katika ushirikiano huo tunapopata wawekezaji na watalii mbalimbali Kuja hapa kwetu nchini, ukisikia wawekezaji wameongezeka au Tanzania imeongeza uuzaji wa bidhàa nje ya nchi Basi ufahamu kuwa Ni matunda ya safari za viongozi wetu wanazofanya huko waendako kazi ya kujenga mahusiano mazuri na wenzetu
Ili Tuendelee tunahitaji kuongeza na kuvutia wawekezaji ambao watasaidia kuongeza wigo wa Kodi na kutoa ajira kwetu vijana, Kodi zitakazo saidia kuboresha huduma mbalimbali za kijamii na kutatua kero mbalimbali