Waziri Mkuu Majaliwa aahidi kuwasomesha Watoto wa Abdulaziz Ahmeid, Mwandishi wa Habari wa Channel Ten aliyefariki

Waziri Mkuu Majaliwa aahidi kuwasomesha Watoto wa Abdulaziz Ahmeid, Mwandishi wa Habari wa Channel Ten aliyefariki

Kwanini hao pekeyake?Watoto wa Daud Mwangosi vipi,nani atawasomesha?
Daudi ni kafiri ...sisi tuna somesha maustadhi ... kama wewe siyo muisiharamu pita [emoji117] kule
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameahidi kuendelea kuwasomesha Watoto wa aliyekuwa mwandishi wa Habari wa Channel Ten, Abdul -Aziz Ahmed ambaye amefariki Dunia Machi 13, 2023 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Majaliwa ametoa ahadi hiyo wakati wa ibada ya kumuaga marehemu Aziz ambapo amesema alikuwa ni moja kati ya waandishi waliokuwa wakiutangaza mkoa huo vizuri. Aziz amepumzishwa katika makaburi ya Mitandi Manispaa ya Lindi.

Aidha, kauli ya Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Lindi, Fatuma Maumba akimzungumzia msibani hapo amesema Abdulaziz Ahmed hakuwa mtu wa kuficha mambo, alikuwa mpambanaji na alifanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na Wadau wengi.



Tuliyasikia pia kwa mdogo wake Aquiline. Lakini kusiwepo utaratibu wa kuwasomesha watu usiokuwa huu wa upendeleo na kujuana kama hivi? Nani wa kuwapiga jeki hawa kwenye hali kama hizi?
 

Attachments

  • 1678457579035.jpg
    1678457579035.jpg
    38.4 KB · Views: 2
Back
Top Bottom