Waziri Mkuu Majaliwa: Corona imepungua Dar na Wagonjwa waliolazwa Wamepungua

Waziri Mkuu Majaliwa: Corona imepungua Dar na Wagonjwa waliolazwa Wamepungua

Mgonjwa wangu kapelekwa icu jana kwa Corona. Looh hawa wanasiasa watatuangamiza
 
Sasa bwashee nitamuamini vipi kama tu jana Hassan Abbas kapeleka vyombo vyote vya habari chaka kwa ku post ndege hewa? Huyu naye muongo tu maana naongea nina uhakika na taatifa zangu bwashee. Huko kambini wamejaa waongo na wapotoshaji ndiyo maana siwasikilizi hata habari zao siwezi kunukuu bwashee.
Lini tunaanza kuokota mizoga barabarani?
 
Lini tunaanza kuokota mizoga barabarani?
Kwa ninavyojua curve ya huu ugonjwa sisi Tanzania tutakuwa kwenye peak mwezi wa tisa. Nadhani nimeshakujibu swali lako. Na nikuonye kuwa peak yetu itakuwa kwenye critical condition upande wa vifo.
Hii ni Science na wasioelewa ndiyo watapata shida sana.
 
Akiongea baada ya swala ya Eid jijini Dodoma, Waziri Mkuu Mh. Majaliwa amesema idadi ya wagonjwa wa Corona imepungua sana nchini.

Amesema hadi leo asubuhi taarifa alizonazo hospitali nyingi hazina wagonjwa na chache zilizobaki wagonjwa wamepungua sana.

Kwa mfano Amana mgonjwa 1, Mloganzila 1, Agakhan 11, Kibaha 16 na Dodoma kuna wagonjwa 3.

Na wagonjwa wote wana hali nzuri wanasubiri kuruhusiwa kasoro Agakhan wagonjwa 4 bado wako katika uangalizi.

Pamoja na yote Mh. Majaliwa amewataka Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari na kuvaa barakoa.

Source: Upendo Tv Habari
kwani ngosha wametumia vipimio vip si machine zenyewe ni mbovu
 
Nature ya huu ugonjwa, kusema mkoa mzima kuna mgonjwa mmoja ni kichekesho.
 
Nisaidieni kumshukuru Mungu. Mjomba wangu Deo, alipata Covid akapambana akapona, bahati mbaya sana mke wake aliyekuwa na ujauzito wa wiki 36 alipata maambukizi. Tarehe 1 mwezi huu alizidiwa na mjomba alizunguka naye kwa masaa 12 akikataliwa kupokelewa kwenye hospitali 6 Dsm. Deo ni mfanyabiasha mdogo sana lakini ameishika sana imani yake. Dakika za mwisho aliamua kwenda Agakhan kujaribu tu, maana pale hupokelewa watu maalum.

Kwa muujiza alipokelewa mkewe akiwa na hali mbaya sana. Kesho yake alifanyiwa operation mtoto akatolewa akiwa mzima. Mama alizidiwa na akakaa ICU kwenye ventilator kwa wiki mbili. Hatimae leo ameruhusiwa kutoka hospitali. Deo ni mtu wa kujitoa sana kwa watu. Bill ilikaribia 40m imechangwa na jamaa na marafiki kupitia group la whatsup alililianzisha.
*Utukufu, Heshima, Mamlaka na Adhama zina wewe MUNGU*
dah ni jambo la kushukuru
 
Akiongea baada ya swala ya Eid jijini Dodoma, Waziri Mkuu Mh. Majaliwa amesema idadi ya wagonjwa wa Corona imepungua sana nchini.

Amesema hadi leo asubuhi taarifa alizonazo hospitali nyingi hazina wagonjwa na chache zilizobaki wagonjwa wamepungua sana.

Kwa mfano Amana mgonjwa 1, Mloganzila 1, Agakhan 11, Kibaha 16 na Dodoma kuna wagonjwa 3.

Na wagonjwa wote wana hali nzuri wanasubiri kuruhusiwa kasoro Agakhan wagonjwa 4 bado wako katika uangalizi.

Pamoja na yote Mh. Majaliwa amewataka Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari na kuvaa barakoa.

Source: Upendo Tv Habari

Sijaelewa hapo idadi ya wagonjwa imepungua kwa kupona au kufariki mbona wanapenda kuongea kimtegokimtego....
 
Inapendeza sana...

Though kwa sasa watu hata wakiugua hawaendi hospitali kwa hofu ya kupimwa Covid19 na kupotezewa muda wakati labda mtu ana homa ya Malaria.

Cc: mahondaw
 
Kwa ninavyojua curve ya huu ugonjwa sisi Tanzania tutakuwa kwenye peak mwezi wa tisa. Nadhani nimeshakujibu swali lako. Na nikuonye kuwa peak yetu itakuwa kwenye critical condition upande wa vifo.
Hii ni Science na wasioelewa ndiyo watapata shida sana.
UK na USA iliwachukua miezi mingapi kufika peak?
 
Back
Top Bottom