“Ngorongoro Mungu aliwapa uwezo wa kukaa na wanyama pamoja hili linavutia na huwezi kuzungumza utalii huu bila ya nyie kuwepo, nikiri mna mchango katika kuongeza pato la taifa kwa uwepo wenu na uhifadhi,” - Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wakazi wa Ngorongoro.
Ameendelea kusema: “Nimekuja hapa kujadili namna ya kutatua changamoto, tunataka watu waishi na watekeleze majukumu yao. Ujio wangu sikuja na malori ya kuja kuwahamisha naomba sana katika kipindi hiki muwe makini, watu wananufaika. Serikali ipo makini na watendaji tupo makini tumeahidi kuwatumikia."
Pia soma
- Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aagiza Wabunge wote waelezwe kinachoendelea Ngorongoro