Waziri Mkuu Majaliwa huu ni mwezi wa nane SGR kipande cha Dar-Moro kinaanza kazi lini?

 
Una hoja ya msingi.
 
Hawa wazembe miaka 5 itapita wako hivi hivi wanaruka ruka tu
 
Hii SGR kukamilika kipande cha Dar-Moro ilishasemwa tangu 2019 na aliyekuwa waziri kamwelwe, kama wameshindwa kukamilisha km. 14 mwaka wa pili huu, vipi km. 1700 kwenda mwanza, vipi km. 1800 kwenda kigoma, vipi km. 1500 kwenda mpanda.......
 
😆😆😆
 
Mnaulizia SGR ya nini, ya kazi gani, kivipi. Si Magu mlimwambia hamtaki maendeleo ya vitu bali demokrasia na uhuru wa kujieleza. Sasa ni kwamba mtatumia demokrasia na uhuru kwenda na kurudi Morogoro

Kwahiyo Magufuli aliacha kujenga hiyo reli akaanza kutekeleza demokrasia?
 
Haya aliyatamka kipindi kile kile alipodanganya msikitini kuwa eti "Magufuli haumwi ila yupo bize na mafaili mengi ofisini" ilihali mwenzie yu hoi huko anapumulia mashine.

Ulikuwa ni "MWEZI WA KUSEMA UONGO KWA WANANCHI - KWA HISANI YA OFISI YA PM".
 
Hapana...tuimarishe demokrasia kwanza. Libya walikuwa na kila kitu ila tu Gadaffi aliwanyima demokrasia wakamtoa. Nasi tunataka demokrasia tu, SGR na Stigla na madaraja ni maendeleo ya vitu yanaweza kusubiri vizazi vijavyo watajenga

Kwahiyo demokrasia ndio inawazuia kumalizia hiyo reli kipande cha Dar-Moro? Umeishiwa hoja za utetezi unaleta uchuro ili upotezee hili swali?
 
Hesabu kuanzia mwaka mmoja mbele ndipo inaweza kuanza kazi.
Ni chizi gani aliyetoa structure ya sgr dar ipite juu?
80% au zaidi ya pesa za mradi zimeishia kwenye kuweka minguzo hapa dar na bado haijakamilika
Lengo lilikuwa ni kuwakoga wapinzani.
 
Acha uongo, walijenga wachina ulikuwa ni msaada.
 
Huyu jamaa si ameshakimbia toka TRC baada ya "kuchoshwa" kuripoti reli kila siku ipo 97% kipande kimekamilika, akaona heshima yake kiuandishi wa habari inashuka.
Huyo dogo alikuwa mwongo sana
 
Hapana...tuimarishe demokrasia kwanza. Libya walikuwa na kila kitu ila tu Gadaffi aliwanyima demokrasia wakamtoa. Nasi tunataka demokrasia tu, SGR na Stigla na madaraja ni maendeleo ya vitu yanaweza kusubiri vizazi vijavyo watajenga
Kama ni hivyo hata demokrasia inaweza kusubiri hadi vizazi vijavyo kama ilivyokuwa kabla ya 1992.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…