Reli ya Tazara ilijengwa na wachina kuanzia mbeba kokoto nk. Mradi wa SGR unazingatia kuwapa Watanzania nafasi kwenye ajira. Angalia wageni kutoka Yapi wako asilimia ngapi? Huwezi kulinganisha na TAZARA. Vile vile zingatia viwanda ambavyo vinajengwa kwa mfano kiwanda cha kutengeneza mataruma ambacho kina Watanzania wengi na uzalishaji huo utakuwa wa muda mrefu . ... .... creating opportunities for Tanzanians.
Sababu nyingine ya kuchelewa ni swala zima la Covid-19. JPM tutakukumbuka sana tu kwa kuona mbali na kutimiza yale ambayo taifa liliamua kufanya. Mwenyezi Mungu amemchukua mapema lakini ameonyesha njia how a country should be governed. Wezi kama JMK na genge lake la wahuni ambao wanafikiria matumbo yao tu siku zao zaja za kulia na kusaga meno. Kumbuka Mwenyezi Mungu hadhihakiwi kwa viumbe wake.
BTW vipande vya Mwanza, Tabora etc vimeanza na huko vitakwenda haraka zaidi kwa sababu mataruma na uzoefu upo mwingi miongoni mwa vijana wa kitanzania.
..Ni kweli walikuja Wachina wengi sana kujenga reli ya Tazara.
..lakini walikuwepo Watanzania wengi zaidi walioshiriki ktk ujenzi huo.
..hoja yangu ni kwamba sasa hivi tuna Vifaa bora zaidi, na utaalamu mkubwa zaidi, kuliko wakati wa ujenzi wa Tazara. Hivyo basi ujenzi wa SGR unatakiwa uende kwa kasi na kwa ufanisi kuliko Tazara.
..Ni kweli kwamba Waturuki wanajenga viwanda mbalimbali vya kusaidia ujenzi wa reli, kwa mfano kiwanda cha mataruma. Uwepo wa kiwanda hicho unatakiwa uongeze kasi ya ujenzi wa reli na sio upunguze kasi.
..Ninavyokumbuka Wachina nao walijenga viwanda mbalimbali vilivyowasaidia ktk ujenzi. Moja ya viwanda hivyo ni kile kilichopo Mang'ula kwa ajili ya mataruma ya reli na ukarabati wa mitambo mbalimbali.
..Kuhusu COVID siwezi kukubaliana na hoja hiyo. Kwanza, reli ya Dar to Moro ilitakiwa iwe imekamilika kabla ya mlipuko wa ugonjwa huo. Pili, ugonjwa huo haujatuathiri Watanzania, na nimesikia viongozi wa serikali wakisema uchumi wetu ilikuwa kuliko wa majirani zetu.
..Mwisho, habari za ujenzi wa vipande vya Mwanza na Tabora umezipata wapi? Taarifa rasmi ni kwamba ujenzi unaendelea kwa vipande vya phase 1 Dar to Moro; phase 2 Moro to Dodoma to Makutupora.
..Pia kuna kipande cha Mwanza to Isaka contract imekuwa awarded sio muda mrefu. Kipande cha Makutupora Tabora Isaka hakina mkandarasi.
..Nadhani serikali na TRC wanapaswa kuwa wawazi zaidi na wakweli kuhusu maendeleo na changamoto za mradi wa sgr.