Waziri Mkuu Majaliwa: Serikali inatafuta njia mbadala za kupunguza gharama za maisha
Sasa ilikuaje Rais akaludisha Tena tozo Tena ya Tsh 100 kwenye Bei ya mafuta Sasa hii kitalamu tuiteje? Wametengeza tatizo halafu wanajadili Tena kuliondoa tatizo in short Serikali haipo sirious na maamuzi yake.
Sababu wao wanapewa bure kila kitu
 
Na bado hadi wese lifike 10,000/= lita ndio akili zitawarudia wadanganyika
 

Yani wanakaa vikao kana kwamba hii bei ya wese walikuwa hawaijui wakati wao ndo waagizaji wa mafuta na ndo watoza tozo....

hii nchi yangu hatupo serious huduma imeshafika Kwenye Jamii ndo mnatafuta suluhu kweli????! Ni too late kweli maana sina hakika kama wanaweza kuishusha bei ya mafuta kwa Hapo ilipo.... na wanasema wameagizwa na raisi wao hawakuona hili kuwa ni tatizo inamaana raisi angekaa kimya ndo imeisha iyo!!! Kasimu Majaliwa na wewe ujitafakari
 
Katelephoni bhna eti sereikl inaendelea kutafuta huku wakipandiha
 
Ila waziri mkuu huaga ana bahati mbaya sana, mambo yake mengine hua yanaendaga kinyume...
 
Bei zetu ni ndogo sana ukilinganisha na U.S'
hapa ndo pakujiuliza..

Na kwa jinsi wanavolishuhulikia hili swala hawaoneshi kbs ile nadharia ya kumfanya kila mtanzania aishi maisha mazuri.

Nadharia inayoonekana wazi ni 'serekali itapata wapi pesa?"

Je hizi pesa zinazotafutwa na serekali ni kwa manufaa ya nani?

Au punda afe mzigo ufike'

Mimi naona hatukuwaza vizuri kuziondoa serikali za kikoloni na zoezi zima la utaifishaji.

Mbona hata wakoloni walifanya mambo mengi tu mazuri kwa maendeleo ya jamii?

Walitudanganya wakoloni ni watu wabaya na wapo kwa ajili ya maslahi yao tu.

Malkia alimuuliza mwalimu, "mtaweza kuiendesha hiyo serekali"?

Malkia alikuwa haoni kabisa kama kweli hawa watu wanaweledi wa kutosha. Na ni kweli hawakuwa na weledi wa kutosha" kuanzia pale ndo tulianza kufeli! Hata mchonga ni mpaka zaidi ya miaka 20 ndo alikuja kujua kwamba hakuna kitu alikuwa anajua.

Na hata mpaka leo bado hawana kbs weledi. Ndo unakuta kiongozi wa ngazi ya juu anaudanganya umma hadharani kabisa, yaani ni waziri lakini tunajua kbs sio mkweli anasema uongo!

Ni bora hata tungeingia mikataba ya kukodishwa hata miaka 100 kama walivyofanya hong kong.

Tungeongozwa na wazungu mpaka sasa tungekuwa mbali sana kuliko hawa wakoloni weusi.

Kule vijijini kuna wazee walisomaga mpaka darasa la 4 chini ya wakoloni.
Wakilewa wanapigaga ngeri tu ilionyooka.
 
Sasa hivi hata wale wachache waliowapigia kura hawana imani tena na utawala wenu. Na yale maneno yenu ya kibehi kuwa tusipokubali ongezeko la tozo tuhamie Burundi.
Shida ni kwamba wanajua blanda wanazofanya, hiyo mikutano ni kujikosha lakini kiuhalisia hakuna cha maana, kesho utasikia mafuta lita 6000
 
Hiyo shilingi 100 tu mliitolea jicho mkairudisha fasta, nasubiri kuona buku ikipunguzwa kwenye hii 3,264 ya dizeli ili tutoe njia kurudi kule kwenye 1800 tulipokuwa awali.
 
IMG-20220505-WA0296.jpg
 
SERIKALI INATAFUTA NJIA MBADALA ZA KUPUNGUZA GHARAMA ZA MAISHA - MAJALIWA
*Aitisha kikao cha kutathmini bei ya mafuta

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali inaendelea kutafuta njia mbadala ambazo zitapunguza gharama ya maisha kwa Watanzania kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia.

"Nawaomba Watanzania waendelee kuwa watulivu na waiamini Serikali yao kuwa tunaendelea kufanya kila linalowezekana ili kuhakikisha tunapunguza gharama za maisha kwa wananchi," amesema.

Waziri Mkuu ametoa wito huo leo (Alhamisi, Mei 5, 2022) katika kikao kilichofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ofisi ndogo ya Waziri Mkuu iliyoko Oysterbay, jijini Dar es Salaam ili kufanya tathmini ya bei ya mafuta na kuangalia namna gani Serikali inaweza kufanya ili kupunguza athari ya bei ya mafuta na kuleta unafuu wa gharama za maisha kwa Watanzania.

Waziri Mkuu amesema kikao hicho kimefanyika ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ameagiza viongozi wa sekta husika wahakikishe wanatafuta suluhisho la kupanda kwa bei ya mafuta hata kama bei hiyo inaendelea kupanda duniani.

"Mheshimiwa Rais ameona changamoto wanayopitia Watanzania kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia, hivyo kikao hiki ni matokeo ya maagizo yake ya kuhakikisha sisi kama viongozi tunatafuta suluhisho la muda mfupi na la muda mrefu ili kukabiliana na changamoto hii," amesisitiza.

Waziri Mkuu amesema kuwa tayari Wizara ya Nishati imeanza kutafuta njia mbadala za uagizaji wa mafuta pamoja na kupunguza makato mengineyo ili kupunguza bei ya mafuta.

"Serikali inaangalia njia mbadala za uagizaji wa mafuta, kupitia kwa wazabuni wengine kama ambavyo imeshauriwa na wabunge na tayari mchakato huo umeanza, kwa kutathmini maombi 24 ambayo yaliwasilishwa kwa Wizara na sasa wamebaki wazabuni sita ambao wameingia hatua inayofuata. Inachokifanya Serikali hivi sasa ni kujiridhisha na uwezo wao wa kusambaza mafuta kulingana na mahitaji na taratibu zilizowekwa na Serikali,” amesema.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Bw. George Simbachawene, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Nishati, Bw. January Makamba, Makatibu Wakuu, pamoja na watendaji wakuu wa taasisi za EWURA, TPDC na Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA).
😍🙏
 
tengeneza tatizo alafu solve tatizo ili kesho useme bila ccm maendeleo hakuna.
alisikika december mikamba
 
Back
Top Bottom