Waziri Mkuu Majaliwa: Tumsaidie Rais Samia kupata wasaidizi waadilifu

Waziri Mkuu Majaliwa: Tumsaidie Rais Samia kupata wasaidizi waadilifu


Huyo waziri mkuu aachane na neno uadilifu maana yuko madarakani kwa kufanya siasa za kishenzi. Huyo ndio aliagiza washindani wake watekwe na kuporwa fomu zao za uchaguzi ili apite bila kupingwa.
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi na waumini waliohudhuria mashindano ya kitaifa ya kuhifadhi Quran tukufu yaliyoandaliwa na taasisi ya Aisha Sururu Foundation (ASF) jijini Dar es Salaam amesema Rais Samia Suluhu Hassan anaguswa na suala la maadili hasa kwa vijana.

"Tunapowahifadhisha Quran vijana wetu, tuhakikishe jambo hilo jema linakwenda sambamba na ujenzi wa misingi imara ya malezi itakayowafanya wawe raia wema, waadilifu na wazalendo kwa nchi yao. Tukiwa wazazi, walezi na walimu wa Quran, nitoe rai kwam-ba tunapotoka hapa hebu tujiulize ni kwa kiasi gani tunaizingatia hi Quran tukufu katika mwenendo mzima wa maisha yetu ya kila siku," amesema na kuongeza;

"Pia tutamsaidia Mheshimiwa Rais kupata wasaidizi wacha Mungu na waadilifu katika kutekeleza majukumu yao ya kuwahudumia wananchi. Majaliwa alihimiza viongozi wa dini kila wanapopata nafasi kwenye mimbari wakemee ukatili wa kijinsia na wale wanaoenda kinyume na maadili na desturi za Kitanzania.

"Nitoe rai kwa viongozi wetu wa dini muendelee kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kulinda mila, desturi na tamaduni za Kitanzania hususan katika kipindi hiki tunachokabiliwa na wimbi kubwa la mmomonyoko wa maadili," alisema.

Majaliwa alisema Tanzania inakabiliwa na tatizo la mmomonyoko wa maadili na pia kumeibuka wimbi la vitendo vingine ambavyo vinakwenda kinyume na dini, mila, desturi na tamaduni za kitanzania.

Yeye ni muadilifu? Huyu ndio kashindwa kusimamia Serikali alikuwa anavimbiwa Hadi na Ma ded wa Mwendazake achilia mbali kina Makonda.
 
Si wapo tayari, kama yule mama wa songea hakuna kitu kila siku anabadilishwa wizara, hivi tunaomba Mungu atusaidiaje pale. Mtu anafahamika ni incompetent yet anapewa wizara tena nyeti kama utumishi.
Mama ana kimzizi sio bure,
 
Back
Top Bottom