#COVID19 Waziri Mkuu Majaliwa: Zoezi la chanjo ya Uviko-19 limefikia zaidi ya asilimia 80

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Dodoma. Waziri wa Mkuu, Kassim Majaliwa amesema zoezi la chanjo ya Uviko-19 limefikia zaidi ya asilimia 80 na zilizobakia mikoani hivi sasa ni chache.

Jumla ya chanjo milioni 1.058 zilizopokelewa nchini kutoka nchini Marekani Julai 24, 2021 na uchanjaji ulizinduliwa rasmi Julai 29, 2021 na Rais Samia Suluhu Hassan.

Kauli hiyo imekuja baada ya Serikali kuanzisha kampeni maalum ya kuhamasisha uchanjaji wa chanjo hiyo katika maeneo mbalimbali ikiwemo makanisani na kwenye mikusanyiko ya watu.

Majaliwa ameyasema hayo leo Jumatatu Oktoba 4 2021, wakati akifungua kongamano la tano la uwezeshaji lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (Neec).

“Tunalo zoezi la uchanjaji. Namshukuru Mungu tumefikia asilimia 80 na kitu huko, tumebaki na chanjo chache sana kwenye mikoa hiyo. Kila mmoja awahi huko na kama kuna mahitaji tutaleta nyingine malengo ni afya,”amesema.

Amesema suala la chanjo sio lazima lakini ni muhimu kwaasababu linasaidia kuongeza virutubisho mwilini na iwapo mtu atapata hawezi kuwa mwepesi kama vile mtu ambaye hajachanjwa kabisa.

Amewaagiza wakuu wa mikoa kutoa elimu na kuhamasisha kuhusu umuhimu wa kuchanja chanjo hiyo.

Mwananchi​

Kwa hiyo unabisha? Watu wanachanjwa kwa wingi mitaani. Hata wenyewe JF wameibuka na hashtag #UjanjaKuchanja.
 
80% ya chanjo 1m zilizopo ni sawa lakini ya chanjo ni tungo tata
 
Kuna hela walichukua kwa mabeberu, ili waongezewe lazima chanjo ziishe. Hata wakiziteketeza/choma hat mbwa/ng’ombe hakuna ushahidi.

Si mnakumbuka wale watakaam walienda kuchoma ng’ombe chanjo na ng’ombe wakafa. Dkt Magufuli sijui yupo wapi.

Ila Mama Samia tunampongeza kwa msimamo wake wa hiari. Ila kuna upupu wa vikaragosi vinadhani eti iwe lazima
 
Alicho nacho ni kipaji. Alipo anadhani sote tumesahau wala hatukumbuki
 
jamaa ongo xana hili yani hizo mil moja zenyewe hata laki tano hazijatumika anasema asilimia themanini duh , aisee basi sawa kuna watu wajinga sana sijapata kuona hasa huyu diblo dibala, ndiomaana alituaminisha aliongea na jiwe kwa simu wakati jiwe lilishakata moto, na cha ajabu aliongelea msikitini. watu hawaogopi kabisa dhambi ya kusema uongo
 
Dodoma. Waziri wa Mkuu, Kassim Majaliwa amesema zoezi la chanjo ya Uviko-19 limefikia zaidi ya asilimia 80 na zilizobakia mikoani hivi sasa ni chache.

Jumla ya chanjo milioni 1.058 zilizopokelewa nchini kutoka nchini Marekani Julai 24, 2021 na uchanjaji ulizinduliwa rasmi Julai 29, 2021 na Rais Samia Suluhu Hassan.

Kauli hiyo imekuja baada ya Serikali kuanzisha kampeni maalum ya kuhamasisha uchanjaji wa chanjo hiyo katika maeneo mbalimbali ikiwemo makanisani na kwenye mikusanyiko ya watu.

Majaliwa ameyasema hayo leo Jumatatu Oktoba 4 2021, wakati akifungua kongamano la tano la uwezeshaji lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (Neec).

“Tunalo zoezi la uchanjaji. Namshukuru Mungu tumefikia asilimia 80 na kitu huko, tumebaki na chanjo chache sana kwenye mikoa hiyo. Kila mmoja awahi huko na kama kuna mahitaji tutaleta nyingine malengo ni afya,”amesema.

Amesema suala la chanjo sio lazima lakini ni muhimu kwaasababu linasaidia kuongeza virutubisho mwilini na iwapo mtu atapata hawezi kuwa mwepesi kama vile mtu ambaye hajachanjwa kabisa.

Amewaagiza wakuu wa mikoa kutoa elimu na kuhamasisha kuhusu umuhimu wa kuchanja chanjo hiyo.

Mwananchi​

Yale yale ya aMagufuli yupo ofisini anachapa kazi
 
Hii historia aijui ka itakuja kusahaulika
 
Hesabu zao tu unajua kabisa chanjo wamezitupa wanafanya siasa.
Huyu kiumbe anaeitwa Majaliwa amekaa muongo muongo mno.
Yaani nchi pekee waziri mkuu muongo ni tz! Yaani msigwa jana anasema wameshachnja laki tano halafu leo wamechanja laki nane yaani siku moja tu watu laki tatu? Uongo wa hali ya juu!
 
Kama ndio hivyo awaambie wasaidizi wake wasitulazimishe kuchanja. Walio chanja wanatosha. Huku Mbeya mkubwa wa Mkoa amesema watapita godoro kwa godoro na makanisani kuwapa watu chanjo
 
Back
Top Bottom