Sumaye aliondoka CCM kwasababu hakukuwa na DEMOKRASIA KATIKA UTEUZI WA WAGOMBEA WA URAIS. Ni kile alichokiita kuwa Kkwete alitumia ubabe kuteua watano awapendao.
Leo anakimbia CHADEMA kwa sababu huko nako hakuna DEMOKRASIA KATIKA UCHAGUZI WA MWENYE KITI WA CHAMA, iliyopelekea yeye kujiondoa na hatimaye kukihama chama.
Karudi CCM ambako M/kiti wa chama hicho hupokezana kwa majina, hakuna kuchukua fomu. Haijatokea hata mara moja na urais ndio asahau kabisa, kwa vile alishatoswa.
Du, pole Mr Zero, maana anatoka chama kisicho na demokrasia na kukimbilia chama kisichona demokrasia kwa muujibu wa maneno yake yeye mwenyewe. Kaogopa hata kuchukua kadi ya CCM nyumbani kwake, badala yake ataifuata Dodoma. Bashiru alijitahidi kulitetea hilo. Tabu kweli kweli!!