Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye arejea CCM, alijiengua CHADEMA baada ya kuambiwa na Mbowe 'Sumu haionjwi kwa kuilamba'

Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye arejea CCM, alijiengua CHADEMA baada ya kuambiwa na Mbowe 'Sumu haionjwi kwa kuilamba'

Safi sana, bado mh. Nyalandu. Baada ya kukamilisha kazi aliyotumwa upinzani, tutamkaribisha nyumbani.#CCM#SISIndioWATAALAM BUANA#
 
Mwenye Sumaye kasema amechoka kubeba maji (CHADEMA) kwenye gunia.
 
Hakuna jipya. Sasa atarudishiwa mali zake zote ikiwa pamoja na mashamba yake. Kilio chake kimesikika.

Kuna wanaume duniani, mpaka Sumaye anapiga magoti. Kisa alishindwa kwenye mbio za URAIS. Sasa karudi nyuma kilomita 1000. Heri kama angempigia makofi toka pale mwanzo. Wachumia tumbo!!!!!!!!!!
 
Hili ni pigo kwa CHADEMA Zero na Manywele wanakijua chama kwa undani most likely wanakuwa debriefed kuhusu chadema strategies. Lazima itakuwa na impact mbaya sana
 
Natafuta ile clip ya video 2015, wakati akiamrisha gwaride la CHADEMA. Mwenye nayo atuwekee
 
Kwani kurudi CCM ndio majibu ya Fredrick Sumaye kwa hoja ya Mbowe "Suma haionjwi kwa kuilamba?" Kwa hiyo yeye amekubali kuwa ni sumu isiyolambwa? Ni yapi majibu yake hasa? Are we simple, or average or critical or great minds?
 
Ngoja tumuilize Slaa kama Sumaye ni Asset. Hatimaye wale aliowakimbia Slaa wamemfuata na mbaya zaidi wapo chumbani wakati yeye yupo sebuleni.
Chongeni tena
FB_IMG_1581491063368.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watarudi wote kwa aliye watuma.
Kubanwa, rushwa na vitisho ni mbinu za MaCCM, hata Sumaye
alizitumia!!
Bye bye!!
 
I wish hawa viongozi wastaafu wangeiga kwa Cleopa Msuya. Kimya utafikiri hayupo, anakula pension yake taratiiiibu
 

Sasa wamerudi kwa wanaojua michongo. CHADEMA ni wanafunzi wa michongo, na wala hawakuwasikiliza Lowasa na Sumaye jinsi ya kuiba. Sumaye alikuwa wazi kuwa niliwashauri kuleni na kipofu hao wananguvu za vyombo vya Dola (polisi, jeshi na TISS), msigombane navyo.

Alimaanisha kuwa watoseni wananchi au wandanganyeni wananchi huku mkichukua pesa toka kwa chama tawala. Mtapata amani nanyi mtakuwa matajiri, vyote havikukubaliwa, ndio kaona ni bora arudi kwa wenye kujua michongo.

Mr Zero, kweli njaa mbaya.
 
Sumaye aliondoka CCM kwasababu hakukuwa na DEMOKRASIA KATIKA UTEUZI WA WAGOMBEA WA URAIS. Ni kile alichokiita kuwa Kkwete alitumia ubabe kuteua watano awapendao.

Leo anakimbia CHADEMA kwa sababu huko nako hakuna DEMOKRASIA KATIKA UCHAGUZI WA MWENYE KITI WA CHAMA, iliyopelekea yeye kujiondoa na hatimaye kukihama chama.

Karudi CCM ambako M/kiti wa chama hicho hupokezana kwa majina, hakuna kuchukua fomu. Haijatokea hata mara moja na urais ndio asahau kabisa, kwa vile alishatoswa.

Du, pole Mr Zero, maana anatoka chama kisicho na demokrasia na kukimbilia chama kisichona demokrasia kwa muujibu wa maneno yake yeye mwenyewe. Kaogopa hata kuchukua kadi ya CCM nyumbani kwake, badala yake ataifuata Dodoma. Bashiru alijitahidi kulitetea hilo. Tabu kweli kweli!!
 
Back
Top Bottom