Salamu wana wa uwanja huu. Nimekuwa najiuliza kwa muda mrefu,nn dhamira ya watu kama Sumaye kwa Watanzania hasa maskini.Huyu bwana amedumu kama Waziri Mkuu wa Tanzania kipindi cha Mzee Mkapa kwa miaka kumi mfululizo, hakutosheka.
Akautaka u Rais 2015, mchakato ukamtema, hakiridhika, akahamia CHADEMA kwa mbwembwe nyingi huku akiponda mchakato uliomuengua katika kinyanganyiro kule CCM.Ikawa usiku, ikawa asubuhi, uchaguzi wa Kanda juzijuzi huko CHADEMA ukambwaga chini, pwaaaaaaa,hakuridhika, akatangaza kujiweka kando na Siasa huku akiwatuhumu CHADEMA hata Serikali kwamba mali zake (mashamba) nk,zilitwaliwa.
Jana babu huyu huyu asokuwa na haya, asojitambua, akautangazia umma wa Watanzania kuwa anarejea CCM huku akiwaponda Wapinzani.Napenda nimweleze Sumaye aka Mr ZERO, ww ni ZERO!na Ujue WATANZANIA SIYO WAJINGA!Kibajaji aliwahi kukuambia "KAMA HUKUSHIBA KWENYE SINIA, HUWEZI KUSHIBA KWA KULAMBA VIDOLE" Dhahiri ww ni babu ulotawaliwa na ubinafsi,chuki na tamaa tele.
Nimwombe mh RAIS JPM, huyu jamaa usimteue hata ujumbe wa nyumba kumi kumi, hafai!Ndo hawa watakuja kuendeleza makundi na mipasuko ndani ya chama chetu kitukufu hasa kipindi hiki kuelekea uchaguzi wa twente twente
Sent using
Jamii Forums mobile app