Kinoamiguu
JF-Expert Member
- Nov 29, 2018
- 17,499
- 25,295
Kila nikimsikiliza akiwa jukwaani nakuja kufahamu kwamba Waziri Mkuu anahutubia kwa mipasho mikali sana huku akiwajibu CHADEMA, ni kama vile haelewi madai ya CHADEMA au anafanya makusudi. Kama ilivyo kawaida yake tangu huko alipotoka. Huyu ni MUHAFIDHINA.
Wakati nchi imevimba kwa yaliyotokea ya mauaji ya watu, tena wakiwa majumbani mwao hapo tarehe 29 October, 2025, bwana Nchemba yeye yupo kwenye mipasho ya kuwajibu CDM? Kana kwamba ndiyo walioua watu, kumbe wauaji wanajulikana kwamba ni SAMIA na vyombo vyake vya dola. Tena yeye akikimbilia NGERENGERE kujificha na JAKAYA. Mulilo alikataliwa na kila mwenye hoteli akaenda kulala LUGALO JWTZ, tunafahamu.
Mfano katika hotuba yake moja, MWIGULU alisema asichokifahamu juu ya madai ya CDM ya kuahirishwa kwa uchaguzi; kwamba CDM walitaka muda wa serikali kukaa madarakani uishe ili waingie barabarani kwa maandamano, tena huku ameshika KATIBA. Huyu ni Waziri Mkuu wa namna gani asiyejua hata Katiba. AIBU.
Nimkumbushe Mwigulu kuwa CDM walipendekeza serikali iongezwe hata mwaka wa kukaa madarakani, yaani mwaka huu wote, ili marekebisho ya sheria za UCHAGUZI na KATIBA yafanyike ndipo uchaguzi uitishwe.
GUYS, GUYS, GUYS, haelewi hili au anapotosha makusudi?
Watu wanaotaka kuandamana kwa serikali kupitisha muda wanakuongezeaje mwaka mzima?
CDM walipendekeza hata kuongezwa kwa muda wa Bunge la BAJETI 2025/26. Japo ni gharama, lakini minimal reforms zifanywe.
GUYS, GUYS, GUYS, huyu PM alikuwa wapi wakati haya yanahubiriwa na HECHE na wenzake, tena wakiwa MAHAKAMANI baada ya kuzuiwa kufanya siasa kwa barua ya Msajili?
GUYS, GUYS.
Mwigulu anakwenda mbali kwa kuwauliza watu, ULIKUWEPO?
Yaani wananchi wasihoji juu ya mauaji ya ndugu zao kwa sababu HAWAKUWEPO? Sisi tulikuwepo. Wakati ndugu, rafiki na jamaa zetu wanauwawa. Mfano mimi nilikuwepo Salasala tu hapo wakati watu wanapigwa shaba wakiwa madukani.
GUYS, GUYS.
Mwigulu wewe hukuwepo kwa kuwa ulikuwa MASAKI na matajiri wenzio.
Mwigulu anasema kuna PESA zimeingizwa toka nje kuja kulipwa waandamanaji? Huyu ni PM wa namna gani anaongea mipasho bila uthibitisho?
GUYS?
Wakati haya yanatokea alikuwa Waziri wa Fedha na anajua taratibu zote za kutuma pesa toka nje ya nchi. Guys, mbona hajawahi kusema waliolipwa walilipwa kupitia mfumo upi wa malipo hata serikali ikashindwa kubaini hayo malipo?
Yaani pesa itumwe toka nje, iingie nchini, watu walipwe, wapangwe kuandamana, waandamane bila serikali kujua?
Sasa hapo kuna serikali au kuna kikundi cha wala rushwa?
GUYS?
Mwisho, washauri wake wamwambie PM siyo KATIBU MWENEZI wa CCM, ni wa Watanzania wote.
Aache kuropoka.