chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,859
- 28,112
Mzee wetu Majaliwa kwa kweli ndio C.E.O, kwa maana ya mtendaji mkuu wa serikali. Kwa nini madudu haya yanatokea na yeye akiwepo? Ameshindwa kusimamia shughuli za serikali?
Bunge linatakiwa limuhoji yeye kwa kuwa Yuko Bungeni kwa niaba ya serikali, na ndiye mtendaji mkuu. Kama hana majibu, walioegesha miti ili jumba bovu lisianguke, wakaitoe.
Hivi anashindwa kuigawa nchi katika Kanda, na Kila Kanda ikawa na usimamizi wake wa moja kwa moja kutoka kwa kikosi kazi Cha kusimamia halmashauri za Kanda hiyo? Kama Hela inatoka, wanachunguza risiti kabisa mapema.
Kama CAG ana Ofisi Kila Mkoa, kwa nini Mkaguzi wa ndani hana?
Kwanini CAG asubiri mwaka mzima ndio atoe ripoti? Kwa nini asifanye hivyo Kila miezi mitatu? Hivyo ya mwaka iwe ya majumuisho?
Kwanini baadhi ya halmashauri na taasisi, kiuhasibu, zisiwekwe karantini ya kiuhasibu, kwa maana kuwa chini ya uangalizi maalum kwa kila wanachofanya? Inaweza kuwa uangalizi wa miaka mitano, mitatu, miwili.
Kwanini shirika na NHIF lisisaidiwe kwa mkakati maalum kuondoa hasara?
Kwanini huwa tunasikia taarifa za Mkaguzi wa nje wa mahesabu (CAG), lakini hatujawahi kumuona Mkaguzi wa ndani akatuambia ilikuwaje malipo fulani akayaidhinisha?