Waziri Mkuu ni kiongozi wa shughuli za Tanganyika hawezi kutoka Zanzibar

Samia ameteua DED, DC hadi RC kutoka Zanzibar kinyume na katiba maana Tamisemi sio wizara ya Muungano na hakuna aliyemkemea wala kumshauri sembuse akiteua Waziri Mkuu ambae katiba inaruhusu. Punguzeni porojo
 
Soma Ibara ya 52, Waziri Mkuu hawezi kulisimamia wala kulidhibiti baraza la Wawakilishi ambalo ndilo linaisimamia serikali ya Zanzibar, je PM mamlaka yake yanaishia wapi Nungwi.
Waziri mkuu ni kiongozi wa serikali kwenye bunge la muungano, baraza la wawakilishi mamlaka yake yanaishia zanzibar wakati bunge la muungano na serikali ya muungano mamlaka yake yanajumuhisha Tanganyika na visiwani.
Rudi kasome katiba ya muungano, mamlaka ya serikali ya muungano utaelewa vizuri.
Kabla ya vyama vingi rais wa Zanzibar alikuwa anahesabika kama makamu wa rais wa serikali ya muungano lakini utaratibu wake ulibadilika baada ya mfumo wa vyama vingi ukichukulia alikuwa akipatikana kwa kuchaguliwa na upande mmoja wa muungano
 
52.-(2) Waziri Mkuu atakuwa Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni.

Bunge ni bunge la JMT tofauti na baraza la Wawakilishi.

106.-(1) Kutakuwa na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar. Linajumuisha wajumbe wanaochaguliwa/kuteuliwa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, pamoja na Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika utekelezaji wa madaraka yake kwa mujibu wa Katiba ya Muungano na Katiba ya Zanzibar.

Ibara hii 106(1) inamtoa Waziri Mkuu, kwahiyo PM hahusiki na utekelezaji wa masuala ya Zanzibar pamoja na kuwa ni PM wa Jamhuri ya Muungano.
 
weka hiko kifungu
Nimeshaweka hapo juu,

52.-(2) Waziri Mkuu atakuwa Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni.

Bunge ni bunge la JMT tofauti na baraza la Wawakilishi.

106.-(1) Kutakuwa na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar ..... pamoja na Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanziba tofauti na kiongozi wa serikali ya JMT.
 
sawa, vipi kuhusu
52.-(1) Waziri Mkuu atakuwa na madaraka juuya udhibiti, usimamiaji, utekelezaji wa siku hata sikuwa kazi na shughuli za Serikali ya Jamhuri yaMuungano.

hapo inampa nguvu zenye mipaka gani
 
Mipaka yake ina mipaka hawezi kulidhibiti baraza la Wawakilishi ibara ya 106.

Waziri Mkuu ni ceremonial PM akiingia Zanzibar sawa na rais wa Zanzibar akija bara/Tanganyika anakuwa kama waziri tu kutoka Zanzibar.
 
  • Thanks
Reactions: Lax

huo ni uhalisia uliowazi, kwahiyo hata yale mambo ya muungano upande ule hana nguvu?
 
52.-(2) Waziri Mkuu atakuwa Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni.

Bunge ni bunge la JMT tofauti na baraza la Wawakilishi.

106.-(1) Kutakuwa na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar. Linajumuisha wajumbe wanaochaguliwa/kuteuliwa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, pamoja na Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika utekelezaji wa madaraka yake kwa mujibu wa Katiba ya Muungano na Katiba ya Zanzibar.

Ibara hii 106(1) inamtoa Waziri Mkuu, kwahiyo PM hahusiki na utekelezaji wa masuala ya Zanzibar pamoja na kuwa ni PM wa Jamhuri ya Muungano.
Mamlaka ya waziri mkuu ni kutohusika na maswala yasiyo ya kimuungano Zanzibar lakini bado anawajibika kwa mambo ya muungano yanayohusu Zanzibar. Soma kwa makini hivyo kamq Zanzibar kuna maswala ya muungano ambayo yapo waziri mkuu anahusika moja kwa moja.
 
Pamoja na katiba kuruhusu Mbunge wa Jamhuri ya Muungano kutoka upande wa Zanzibar kuwa Waziri Mkuu lkn kunaweza kuwa na mgongano wa kimaslahi pengine kikatiba.

Ibara ya 66(1) inasema wajumbe wa Baraza la Wawakilishi miongoni mwao wanaweza pia kuwa Wabunge wa Muungano.

Moja ya wajibu wa Waziri Mkuu ni kusimamia na kudhibiti utekelezaji wa shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano, ambapo Zanzibar ni eneo lake la kazi kikatiba, lakini hana mamlaka ya kulidhibiti Baraza la Wawakilishi.

Ikitokea Waziri Mkuu wa JMT ambaye pia ni mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kutokana na Ibara ya 66(1), hawezi kudhibiti shughuli za Baraza Wawakilishi ambalo kazi yake ni pamoja na kutunga sheria za Zanzibar, hatuoni kuwa kuna mgongano wa kimaslahi.

Ndio maana nasema kwa katiba hii ni vigumu sana kuwa na Waziri Mkuu kutoka Zanzibar hasa kwa situation tuliyo nayo ambapo Rais na Makamu wake wote ni Wazanzibari.
Kama Kuna Wakuu wa wilaya wazanzibar na mawaziri wazanzibar kwenye wizara zisizo za Muumgano, lolote linaweza tokea.
 
Hakuna kisichowezakana tena hii Tanzania, rais ajaye anaweza kuwa Rizimoko wa Msoga
 
Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania anaweza kuteuliwa kutoka Zanzibar au bara ilimradi awe wa kuchaguliwa na cyo viti maalum
Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania atasimamia na kudhibiti shughuri za jamhuri ya muungano pekee hana mamlaka na baraza la wawakilishi
 
Pamoja na katiba kuruhusu Mbunge wa Jamhuri ya Muungano kutoka upande wa Zanzibar kuwa Waziri Mkuu lkn kunaweza kuwa na mgongano wa kimaslahi pengine kikatiba.

Ibara ya 66(1) inasema wajumbe wa Baraza la Wawakilishi miongoni mwao wanaweza pia kuwa Wabunge wa Muungano.

Moja ya wajibu wa Waziri Mkuu ni kusimamia na kudhibiti utekelezaji wa shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano, ambapo Zanzibar ni eneo lake la kazi kikatiba, lakini hana mamlaka ya kulidhibiti Baraza la Wawakilishi.

Ikitokea Waziri Mkuu wa JMT ambaye pia ni mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kutokana na Ibara ya 66(1), hawezi kudhibiti shughuli za Baraza Wawakilishi ambalo kazi yake ni pamoja na kutunga sheria za Zanzibar, hatuoni kuwa kuna mgongano wa kimaslahi.

Ndio maana nasema kwa katiba hii ni vigumu sana kuwa na Waziri Mkuu kutoka Zanzibar hasa kwa situation tuliyo nayo ambapo Rais na Makamu wake wote ni Wazanzibari.
Ngoja nikukumbushe. Ipo hivi. Jamhuri ya Muungano ina pande mbili, Tanzania na Zanzibar.
Katika nafasi mbalimbali kuna nafasi za Muungano na zisizo za Muungano.
Mfano wa Wizara zisizo za Muungano ni Wizara ya Rlimu, Afya, Utalii, Kilimo, Nishati na Miundombinu Ardhi, Maji na TAMISEMI.

Wizara hizi hazifanyi kazi upande wa Zanzibar. Zinaishia upande wa hara. Sifa za wanaofanya kazi katika Wizara hizi sharti ni kuwa Watanzania, hivyo nafasi yoyote ambayo siyo ya Muungano, Mzanzibar anaweza kuteuliwa kuishika sababu ya Utanzania wake. TAMISEMI kujaa wazanzibar, Ma DASS, Wakuu wa Mikoa, RAS, Wakuu wa Wilaya n.k, pia kuna wizara zinazosemekana kuwa siyo za Muungano lakini zinaongozwa na Wazanzibar. Muungano wa kipuuzi kabisa huu.

Upande wa Zanzibar Katiba yao ipo wazi, inaongelea Mzanzibar na ina vitu vinavyomtambulisha Mzanzibar.
Upande wa bara haupo, kuna upande wa Jamhuri ya Muungano, huko nafasi watu hupewa kwa utanzania wao, siyo Utanganyika. Hata kama kuna sehemu itaongelea habari za upande wa pili wa Muungano, ni geresha tu, itakuwa inajichanganya sababu haina methodology ya kuwatofautisha watanzania wa upande mmoja na mwingine, kwake Watanzania wote ni sawa wana uwezo wa kufanya kazi popote..

Tukija kwenye hoja yako, imekaa kimazoea tu, kwani akuteuliwa Mzanzibar kuwa Waziri Mkuu sehemu gani ya Katiba itakuwa imevunjwa?
 
Mamlaka ya waziri mkuu ni kutohusika na maswala yasiyo ya kimuungano Zanzibar lakini bado anawajibika kwa mambo ya muungano yanayohusu Zanzibar. Soma kwa makini hivyo kamq Zanzibar kuna maswala ya muungano ambayo yapo waziri mkuu anahusika moja kwa moja.
Katiba inasema hivyo ila utekelezaji wake ni mgumu, mfano bandari, kodi, ni mambo ya Muungano lkn Waziri mkuu hana mamlaka ya kuhoji mambo ya bandari za Zanzibar.

Kumbuka baraza la Wawakilishi linasimamia shughuli zote za Zanzibar.
 
on paper hizo bandari za zenji zinatakiwa zisimamiwe na serikali ya muungano, kwa asilimia kubwa muungano upande wa zenji ulishakwisha kwenye mambo mengi sana
 
Pamoja na katiba kuruhusu Mbunge wa Jamhuri ya Muungano kutoka upande wa Zanzibar kuwa Waziri Mkuu lkn kunaweza kuwa na mgongano wa kimaslahi pengine kikatiba.

Ibara ya 66(1) inasema wajumbe wa Baraza la Wawakilishi miongoni mwao wanaweza pia kuwa Wabunge wa Muungano.

Moja ya wajibu wa Waziri Mkuu ni kusimamia na kudhibiti utekelezaji wa shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano, ambapo Zanzibar ni eneo lake la kazi kikatiba, lakini hana mamlaka ya kulidhibiti Baraza la Wawakilishi.

Ikitokea Waziri Mkuu wa JMT ambaye pia ni mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kutokana na Ibara ya 66(1), hawezi kudhibiti shughuli za Baraza Wawakilishi ambalo kazi yake ni pamoja na kutunga sheria za Zanzibar, hatuoni kuwa kuna mgongano wa kimaslahi.

Ndio maana nasema kwa katiba hii ni vigumu sana kuwa na Waziri Mkuu kutoka Zanzibar hasa kwa situation tuliyo nayo ambapo Rais na Makamu wake wote ni Wazanzibari.
Waziri Mkuu ni Mkuu wa Tanganyika, hivyo kamwe hawezi kutokea Zanzibar. Kila unapoona neno Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniapigia mstari kwamba hiyo ni Tanganyika katika jiba la ubatizo.
 
Waziri mkuu ni kiongozi wa serikali kwenye bunge la muungano, baraza la wawakilishi mamlaka yake yanaishia zanzibar wakati bunge la muungano na serikali ya muungano mamlaka yake yanajumuhisha Tanganyika na visiwani.
Rudi kasome katiba ya muungano, mamlaka ya serikali ya muungano utaelewa vizuri.
Kabla ya vyama vingi rais wa Zanzibar alikuwa anahesabika kama makamu wa rais wa serikali ya muungano lakini utaratibu wake ulibadilika baada ya mfumo wa vyama vingi ukichukulia alikuwa akipatikana kwa kuchaguliwa na upande mmoja wa muungano
Hayo hapo kwenye bolt ni nadharia kama ya uwepo wa moto wa milele lakini kwenye utekelezaji mambo hayapo hivo. Kila unapoona neno Jamhuri ya Muungano anayesemwa hapo ni Tanganyika. Bunge la Muungano mamlaka yake kwenye utendaji haalisi yaanaishia pale Mogogoni nyuma ya Ikulu ya Tanganyika pale Darusalama. Hata Rais wa Jamhuri ya Muungano (a.k.a Tanganyika) akienda kwenye shughuli za maadhimisho Zanzibar anabana miguu wakati Rais wa Zanzibar na Mkuu wa Nchi ya Zanzibar aakipigiwa Mizinga 21 ya Kijeshi. Ukijifanya kuyajua sana mambo ya Tanzania na CCM utachanganyikiwa bure.
 
Back
Top Bottom