Waziri Mkuu ni kiongozi wa shughuli za Tanganyika hawezi kutoka Zanzibar

Kwan Zanzibar ni nchi au nchi ndani ya nchi
Nijibiwe haya maswali.
1.kuna nchi isiyo na jeshi ? Zanzibar Ina jeshi kama lipo, nan amiri jeshi mkuu wake?
2.Naomba kufaham mkuu wa majeshi ya Zanzibar ?
3.Kitiifaki kati ya rais wa Zanzibar na makamo wa rais muungano nan mkubwa ?
4. Ni wakati gan rais wa Zanzibar atakuwa na mamlaka KWENYE serikari ya muungano?
5.Ktk baraza la usala wa taifa rais wa Zanzibar anaingia kama nan? Na makamo wa rais muungano anaingia kama nan ?
Na makamo mwenyekiti wa baraza Hilo ni nan?

Huu muungano alieusuka alikosea vitu vingi sana
 
Katiba inasema hivyo ila utekelezaji wake ni mgumu, mfano bandari, kodi, ni mambo ya Muungano lkn Waziri mkuu hana mamlaka ya kuhoji mambo ya bandari za Zanzibar.

Kumbuka baraza la Wawakilishi linasimamia shughuli zote za Zanzibar.
Umeongea vyema hapa mambo mengi wanayafanya kienyeji hawazingatii katiba.
 
Kama ungefatilia kesi ya uhaini waliyopewa viongozi wa CUF usingeuliza hayo maswali, Zanzibar hauwezi kufanyika uhaini sababu Zqnzibar siyo dola. Kwa lugha nyingine Zanzibar haina jeshi wa amiri mkuu wa majesho.
 
Katiba ndio mwongozo wa kila kitu
 
Watanganyika hata akitoka Malawi hawanaga shida

Cha MSINGI uwe unawapa connection mpya Kila mara na taarifa za wajawazito watu maarufu
 
Katiba ndio mwongozo wa kila kitu
Katiba hii hii ambayo hadi wazanzibar wanapewa nafasi za uongozi katika Wizara zisozo za Muungano? Katiba hii ambayo Chama kimoja kinaweza kujitangazia ushindi wa hadi asilimia 98? Katiba hii hii ambayo Mama yetu anaita Kijitabu tu???

Kwa ufupi Katiba kwa nchi zilizostaarabika tu. Kwa nchi zetu watawala wapo juu ya Katiba na Sheria.
 
Katiba hairuhusu hayo mambo tatizo katiba yetu haina kinga ndio maana rais anajiamlia anavyotaka akijua hawezi kubanwa kisheria akivunja katiba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…