Waziri Mkuu ni lazima awe Mtanganyika?

Waziri Mkuu ni lazima awe Mtanganyika?

Kwanini Wazanzibar mnatamaa hivi? Rais katoka kwenu na PM mnataka lakini hamchangii chochote kwenye budget ya nchi, watanganyika hata kuwa Mwenyekiti wa mtaa Zanzibar haiwezekani nyie mnataka vyote.
 
Hata Rais wa Tanganyika anatakiwa awe Mtanganyika. Na huu ndiyo ukweli mchungu. Haiwezekani nchi iliyopata uhuru wake 9/12/1961 iongozwe na mtu kutoka nchi nyingine.

NB: niko tayari kukosolewa kama sipo sahihi. Hapa naongelea Tanganyika. Na siyo Tanzania Bara.
Huu muungano fake uvunjwe haraka bara tumegeuzwa koloni la Zanzibar asee
 
Ndio ni lazima awe Mtanganyika, kwa kifupi sana TAMISEMI ndio kama serikali ya watu wa Tanganyika na hata viongozi na ajira zake zinapasa kuwa za Watanganyika.

Ila somo la uraia liangaliwe upya kinachofundishwa maana watu hawaujui kabisa muundo wa taifa lao
 
Cheo cha makamu hakina nguvu wabaki nacho wazenji. Wao kule wana serikali yao
Hoja yako Numbisa nimeielewa. Kwa kuwa wao wana Serikali Yao, huku kwenye Muungano wawe wanatoa makamo wa Rais na Rais atoke Tanganyika.
 
Waziriki mkuu anatakiwa awe Mtanzania, Tanganyika haipo mkuu. Kwahiyo hata akitoka Visiwani naye pia ni Mtanzania
 
Tangu mwaka 1964 Tanganyika na Zanzibar ziungane, ni Salim Ahmed Salim tu aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania.

Zaidi ya Salim Ahmed Salim hakuna mzanzibari mwingine aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania.

Je, cheo cha uwaziri Mkuu ni cha Muungano au ni kwa ajili ya watu wa Tanganyika?

Kama ni kwa ajili ya watu wa Tanganyika, ilikuwaje Salim Ahmed Salim alipata kuwa Waziri Mkuu?

Kuna watu wanadai kuwa waziri Mkuu ni nafasi ya kisiasa kwa ajili ya kulinda maslahi ya Tanganyika ndani ya Serikali ya Muungano. Ni kweli?
Kwani rais wa Baraza la Mapinduzi anaweza kuwa mtanganyika? Yaani mnataka urais na uwaziri mkuu! Kiinchi chenyewe kipande kisicholingana na wilaya ya Mkuranga. Tuondolee tamaa na kutaka kutugeuza mazwazwa.
 
He..!! Wazanzibari sasa wanautaka na Uwaziri mkuu.. Ya kushangaza hayataisha..
 
Sasa kama Azimio la Lindi lilikataa Waziri mkuu kuwa Rais inakuwaje mawaziri wakuu huwa wanautaka Urais kwa nguvu zote..??

Rejea: Salim, Malecela, Msuya, Sumaye, Lowasa..

Si bora wasingepoteza fedha na nguvu zao..
 
Back
Top Bottom