Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewasilisha ujumbe mzito kutoka kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisisitiza kuwa mkuu huyo wa nchi hapendi na wala havumilii vitendo vya rushwa, ubadhirifu wa mali za umma, na uzembe kazini.
Dkt. Mwigulu ameyasema hayo leo, Januari 26, 2026, mkoani Morogoro, alipokuwa akimwakilisha Rais katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Akizungumza na viongozi hao wa TAKUKURU, Waziri Mkuu amebainisha kuwa dhamira ya Rais Samia ya kulinda utu wa mwananchi na kuhakikisha maendeleo ya taifa inategemea sana uadilifu na uwajibikaji wa taasisi za udhibiti. Ameeleza kuwa Rais amekuwa akifanya juhudi za makusudi kuziimarisha taasisi hizo kwa kuziongezea rasilimali watu, bajeti, miundombinu, na hata kufanya marekebisho ya kisheria ili kuzipa "meno" ya kutosha kutekeleza majukumu yao.
Waziri Mkuu ameongeza kuwa kupitia kazi nzuri inayofanywa na TAKUKURU, rasilimali za nchi zitatumika ipasavyo kwa ajili ya kuwaletea Watanzania maendeleo ya kweli. Amewataka viongozi hao kupokea salamu za Rais na kuendelea kupambana na vitendo vyote vinavyoharibu misingi ya utawala bora, huku wakijua kuwa wana uungaji mkono wa asilimia 100 kutoka ngazi ya juu ya uongozi wa nchi.