Waziri Mkuu: Rais Samia anachukia rushwa na ubadhirifu wa mali

Waziri Mkuu: Rais Samia anachukia rushwa na ubadhirifu wa mali

Mkuu nyingi zinazoandikwa kuhusiana na Samia ni uzushi wa mitandaoni unaotokana na chuki pamoja na ubaguzi dhidi ya SSH kwamba ni mwanamke mzenji anayeiongoza TZ, hicho kitu huku bara wengi hawapendi.

Inapokuwepo chuki na ubaguzi ni rahisi kutengeneza habari za kizushi katika kuichafua taswira ya kiongozi, hao wenye chuki na ubaguzi wanakuwa na huo msukumo wa kuitenda dhambi bila ya wao wenyewe kujua kwamba wanachokifanya ni dhambi.

Huu nao ukenge mwengine wa wazi, yani watu wasimpende ntu kwa kuwa ni mwananke? Wanawake tunawapenda(ga) sana mbona. Au kwa kuwa mzanzibara? Mbona alikuwepo mzee Mwinyi, Salim Ahmed Salim na Aboud Jumbe wkt bado unanyonya? Umediocre wake na nepotism na uuaji huenda ndio sababu I guess. Nyerere pamoja na kuchukua hii nchi ikiwa na watu hata kaptula hawaijui na ukenge mkubwa zaidi hajawahi kumuweka mwanae waziri, zaidi alimpleka vitani kabisa wala mkwewe, kwani hakuona hizo nafasi? Huyu mama angeweka wanae na wakwe zake kuwa wakurugenzi sehemu si wangepiga tu kuliko hii dharau kwa kila kenge eti mwanae waziri, mkwe waziri, mshenga waziri, kijana muuza tyres kariakoo mara bilionea wa ghafla, nk nk!

Hamna anayemchukia, period
 
Mkuu nyingi zinazoandikwa kuhusiana na Samia ni uzushi wa mitandaoni unaotokana na chuki pamoja na ubaguzi dhidi ya SSH kwamba ni mwanamke mzenji anayeiongoza TZ, hicho kitu huku bara wengi hawapendi.

Inapokuwepo chuki na ubaguzi ni rahisi kutengeneza habari za kizushi katika kuichafua taswira ya kiongozi, hao wenye chuki na ubaguzi wanakuwa na huo msukumo wa kuitenda dhambi bila ya wao wenyewe kujua kwamba wanachokifanya ni dhambi.
Kwahiyo kura 31m ni kweli ila watu hawataki maana yeye ni mwanamke na mzanzibar?
 
Kwahiyo kura 31m ni kweli ila watu hawataki maana yeye ni mwanamke na mzanzibar?
SSH anafanya mengi huko mikoani, sisi huku DSM hatuwezi kuliona hilo kwa sababu tunamezwa na chuki.

Kule Ziwa Victoria imeanza kazi meli ya kutoka Mwanza kwenda Bukoba, kwanini wakazi wa kule wamnyime kura?.

Kuna daraja la busisi kwanini watumiaji wamnyime kura? kwanini wavuvi wanaofaidika na kiwanda cha samaki Lindi wamnyime kura?.
 
SSH anafanya mengi huko mikoani, sisi huku DSM hatuwezi kuliona hilo kwa sababu tunamezwa na chuki.

Kule Ziwa Victoria imeanza kazi meli ya kutoka Mwanza kwenda Bukoba, kwanini wakazi wa kule wamnyime kura?.

Kuna daraja la busisi kwanini watumiaji wamnyime kura? kwanini wavuvi wanaofaidika na kiwanda cha samaki Lindi wamnyime kura?.
Hivyo vitu vinafanywa na kodi za watanzania sio mshahara wa Samia, watu wanatoa kura kwa wamtakaye sio aliyeko madarakani. Narudia tena kura 31m ni za kweli?
 
Hivyo vitu vinafanywa na kodi za watanzania sio mshahara wa Samia, watu wanatoa kura kwa wamtakaye sio aliyeko madarakani. Narudia tena kura 31m ni za kweli?
Kwanini ziwe takwimu za uongo wakati hizo nimekutajia ndio sababu zinazompa kura rais?.

Kufanywa na kodi sio issue wapo wanaoshindwa hata kukusanya hizo kodi.
 
Uongo,uongo,uongo,uongo,uongo,uongo,uongo,uongo,uongo,uongo,uongo,uongoooooooooooooooooooooooooo
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewasilisha ujumbe mzito kutoka kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisisitiza kuwa mkuu huyo wa nchi hapendi na wala havumilii vitendo vya rushwa, ubadhirifu wa mali za umma, na uzembe kazini.

Dkt. Mwigulu ameyasema hayo leo, Januari 26, 2026, mkoani Morogoro, alipokuwa akimwakilisha Rais katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Akizungumza na viongozi hao wa TAKUKURU, Waziri Mkuu amebainisha kuwa dhamira ya Rais Samia ya kulinda utu wa mwananchi na kuhakikisha maendeleo ya taifa inategemea sana uadilifu na uwajibikaji wa taasisi za udhibiti. Ameeleza kuwa Rais amekuwa akifanya juhudi za makusudi kuziimarisha taasisi hizo kwa kuziongezea rasilimali watu, bajeti, miundombinu, na hata kufanya marekebisho ya kisheria ili kuzipa "meno" ya kutosha kutekeleza majukumu yao.

Waziri Mkuu ameongeza kuwa kupitia kazi nzuri inayofanywa na TAKUKURU, rasilimali za nchi zitatumika ipasavyo kwa ajili ya kuwaletea Watanzania maendeleo ya kweli. Amewataka viongozi hao kupokea salamu za Rais na kuendelea kupambana na vitendo vyote vinavyoharibu misingi ya utawala bora, huku wakijua kuwa wana uungaji mkono wa asilimia 100 kutoka ngazi ya juu ya uongozi wa nchi.

What a sonofabitch! “Samia anachukia rushwa, anachukia ubadhilifu, anachukia matumizi mabaya ya raslimali za nchi hii, […]”, my foot!
 
Hatujasikia akifuta Kibali cha Watendaje wake KULA KWA UREFU WA KAMBA!
 
WAZIRI MKUU: SERIKALI IMEIMARISHA TAKUKURU KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeimarisha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa kuongeza rasilimali watu, bajeti, miundombinu na kufanya marekebisho ya kisheria ili kuongeza ufanisi wa mapambano dhidi ya rushwa.

Amesema kwa juhudi hizo, TAKUKURU imeokoa zaidi ya shilingi bilioni 60.2, ambazo zimeelekezwa katika huduma muhimu za jamii zikiwemo afya, elimu, maji, umeme na miundombinu. Pia, katika kipindi cha Julai hadi Desemba 2025, Jamhuri imeshinda asilimia 68.8 ya kesi 489 zilizofikishwa mahakamani, ikionyesha ubora wa uchunguzi na ushirikiano kati ya TAKUKURU na Mahakama ya Tanzania.

“Rushwa inadhalilisha utu wa binadamu na inazorotesha utoaji wa huduma za jamii. Ni lazima tuchukue hatua za kuzuia kabla haijazalisha madhara. Rushwa ni ajenda ya kitaifa inayohusu pande zote za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisisitiza Dkt. Nchemba.

Ameyasema hayo leo Jumatatu, Januari 26, 2026, wakati alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Viongozi wa TAKUKURU unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Cate Convention Centre, mkoani Morogoro.

Aliongeza kuwa taasisi za Serikali lazima zibainishe na kuziba mianya ya rushwa hususan katika maeneo ya manunuzi ya umma, utekelezaji wa miradi, na usimamizi wa mikataba, kwani zaidi ya asilimia 75 ya bajeti ya Serikali hupitia katika maeneo hayo. Waziri Mkuu pia aliwahimiza Watanzania kushirikiana na TAKUKURU kwa kutoa taarifa za vitendo vya rushwa, akisisitiza usiri wa watoa taarifa. Aidha, aliwahimiza kushirikisha sekta binafsi, wadau wa kimataifa, pamoja na vijana na wanawake katika jitihada za kupambana na rushwa.

Dkt. Nchemba alisisitiza kuwa Serikali iko tayari kufanya marekebisho ya kisheria na kiutawala pale itakapobainika kuna vikwazo vinavyoathiri utekelezaji wa majukumu ya TAKUKURU, akiwataka viongozi wa taasisi hiyo kuwasilisha mapendekezo yao bila kusita. Pia aliagiza ushirikiano wa karibu kati ya TAKUKURU na Tume ya Maadili ya Utumishi wa Umma ili kuimarisha uadilifu na uwajibikaji katika utendaji wa watumishi wa umma.

Aidha, Waziri Mkuu alielekeza taasisi za Serikali kubaini na kuziba mianya ya rushwa hususan katika maeneo ya manunuzi ya umma, utekelezaji wa miradi, na usimamizi wa mikataba, akibainisha kuwa maeneo haya yanahitaji uangalizi wa karibu kutokana na asilimia kubwa ya bajeti ya Serikali kupitia hapo.

Akisisitiza mwelekeo wa Taifa, Dkt. Nchemba aliunganisha jitihada za TAKUKURU na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, akibainisha kuwa mapambano dhidi ya rushwa ni msingi wa kuimarisha ustawi wa wananchi, maendeleo endelevu, uadilifu, na uwajibikaji wa Taifa. Vilevile, aliangazia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2025–2030, ambayo inaweka wazi mapambano dhidi ya rushwa kama nguzo muhimu ya demokrasia, utawala bora, na ustawi wa wananchi.

Waziri Mkuu alimalizia hotuba yake kwa kutoa wito kwa viongozi wa TAKUKURU kuhakikisha mafanikio yaliyopatikana yanakuwa chachu ya kuongeza bidii zaidi, huku akisisitiza kaulimbiu ya mkutano:

“Kuzuia Rushwa ni Jukumu Lako na Langu; Tutimize Wajibu Wetu.”

Baada ya hotuba hiyo, Waziri Mkuu alitangaza rasmi ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka 2025 wa Viongozi wa TAKUKURU.
 

Attachments

  • IMG-20260126-WA0039.jpg
    IMG-20260126-WA0039.jpg
    328.1 KB · Views: 21
  • IMG-20260126-WA0038.jpg
    IMG-20260126-WA0038.jpg
    387 KB · Views: 20
  • IMG-20260126-WA0041.jpg
    IMG-20260126-WA0041.jpg
    488.2 KB · Views: 15
  • IMG-20260126-WA0040.jpg
    IMG-20260126-WA0040.jpg
    526.5 KB · Views: 14
  • IMG-20260126-WA0042.jpg
    IMG-20260126-WA0042.jpg
    570.7 KB · Views: 18
  • IMG-20260126-WA0037.jpg
    IMG-20260126-WA0037.jpg
    440.6 KB · Views: 19
  • VID-20260126-WA0030.mp4
    30.9 MB
Neno 'serikali' linatumika vibaya sana
huyu pimbi hajui maana ya serikali kweli?
au serikali ni kikundi cha wahuni wachache?

Very sad!
 
Back
Top Bottom