Waziri Mkuu: Tsh. Trilioni 10.69 zimetumika kujenga Reli ya SGR Dar mpaka Moro

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Serikali imeendelea kutoa fedha za utekelezaji wa ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa (SGR) wa kilomita 1,219, kwa kutoa jumla ya Sh10.69 trilioni na kwa ujenzi wa kipande cha Dar es Salaam โ€“ Morogoro.

Soma pia: Uzi mkuu unaoonesha yaliyojiri kwenye mradi wa SGR tangu kuanza kwake mpaka mradi ulipofikia hivi sasa

Hayo yamesemwa leo Jumatano, Aprili 3, 2024 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akisoma mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na ofisi ya Bunge kwa mwaka 2024/2025.

MWANANCHI
 
Dar moro ni km ngapi? KWA njia ya reli. Ili tupate wastani
 
Duuuuh.
Huu mpunga ungetumika kujenga wastani wa Km 10,000 za lami.
 
Uuuwiiiii!
 
Sidhani kama PM ameeleweka ktk hili. Siamini kama hii 10tr ya kipande cha Dar -Moro pekee.

Vv
 
Huyu naye kama huwaga haelewi vitu! Kwani gharama ya reli nzima ni trillion Mia ngapi? Aache Undundu!
 
Tukihoji sana hizo gharama tutajulishwa kuwa aliteleza ulimi... Tukikaa kimya watakaa kimya na kupiga cha juu
 
Hahahaha dah,, ila serikalini pesa ipo, alafu mnaambiwa mjiajiri๐Ÿ˜‚,,

Maji shida
Umeme shida
Barabara shida

Angalau kidogo sehem za town,, lakini kule village KIVUMBI๐Ÿ˜“
 
Hizo ni jumla ya fedha zilizotolewa kwa vipande vyote vilivyo katika % tofauti ya utimilifu na si kwa kipande kimoja cha dar-moro
 
Hii nchi ina laana ya asili
 
Dar to Moro 10.
Moro to Dom 10.
Dom to Singida 10.
Singida to Mboka 10.
Mbokato to Shy 10.
Shy to R.City 10.

zaidi ya trilion 70 zitaungua kwa kukosa maarifa.
Yesu kristo wa Nazareth ๐Ÿ™Œ๐Ÿ™Œ๐Ÿ™Œ๐Ÿ™Œ
 
mbona mwendazake alimaliza malip ya dar dodom jamn haya tenha wap
 
gha
gharama za jumla ndio trilioni 10.69 ila ya moro ni 3. something..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ