PostGE2025 Waziri Mkuu: Tume ya Uchunguzi ya matukio ya Oktoba 29 ni Tume ya Watanzania

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema uundwaji wa tume ya kuchunguza matukio yaliyotokea siku na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 ni hatua muhimu ya kitaifa, akisisitiza kuwa tume hiyo ni ya Watanzania na imeundwa kwa masilahi ya nchi, si kwa malengo ya kisiasa.

Ametoa rai hiyo Jumatatu jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake kukagua athari za matukio hayo, akisisitiza tume hiyo imeundwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuzingatia ukubwa wa tukio, ambalo pamoja na kuharibu miundombinu, limegharimu maisha ya watu wakiwemo wasiokuwa na hatia.

Dkt. Mwigulu amesema tume iliyopewa jukumu la kuchunguza matukio hayo inaundwa na wazee wenye heshima, maarifa na uzoefu mpana katika masuala ya nchi akibainisha kuwa ni “senior citizens” ambao wameaminika na taifa kutokana na mchango wao kwa miaka mingi.

Ameitaka jamii yote kutoa ushirikiano kwa tume, ikiwemo kutoa taarifa, ushahidi na maoni yatakayosaidia kufichua ukweli na kuwezesha hatua stahiki kuchukuliwa.

Pia Soma: Rais Samia aunda Tume ya Uchunguzi wa matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi 2025
 
🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮

20251124_094200.png
 
Tume iliyoteuliwa na mtuhumiwa, na isiyoakisi jamii ya watanzania sio tume huru wala shirikishi.
  • Mwakilishi wa GenZ yuko wapi?
  • Mwakilishi wa mawazo mbadala yuko wapi?
  • Mwakilishi wa wanaosimamia ukweli na haki, taasisi za kiimani wako wapi?
Utapeli mtupu. Hadi kwenye maafa. Hii sio Serikali ya wananchi.
 
🤣🤣🤣🤣 Samia hakuona watu wanachana mabango ya picha zake
 
Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema uundwaji wa tume ya kuchunguza matukio yaliyotokea siku na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 ni hatua muhimu ya kitaifa, akisisitiza kuwa tume hiyo ni ya Watanzania na imeundwa kwa masilahi ya nchi, si kwa malengo ya kisiasa.

Ametoa rai hiyo Jumatatu jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake kukagua athari za matukio hayo, akisisitiza tume hiyo imeundwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuzingatia ukubwa wa tukio, ambalo pamoja na kuharibu miundombinu, limegharimu maisha ya watu wakiwemo wasiokuwa na hatia.

Dkt. Mwigulu amesema tume iliyopewa jukumu la kuchunguza matukio hayo inaundwa na wazee wenye heshima, maarifa na uzoefu mpana katika masuala ya nchi akibainisha kuwa ni “senior citizens” ambao wameaminika na taifa kutokana na mchango wao kwa miaka mingi.

Ameitaka jamii yote kutoa ushirikiano kwa tume, ikiwemo kutoa taarifa, ushahidi na maoni yatakayosaidia kufichua ukweli na kuwezesha hatua stahiki kuchukuliwa.
It’s hard to imagine that hii tume (ikibaini kwamba aliyeiteua ndiye actually aliyesababisha taifa kuingia kwenye machafuko) itasema Rais ndiye alikuwa chanzo cha hayo machafuko. That’s mission impossible!
 
Ya mtuhumiwa kujichunguza?.
Samia hana moral authority ya kuunda tume kwani naye ni mtuhumiwa.
 
Wanatuchukuliaje lakini hawa🙆‍♂️🙆‍♂️🙆‍♂️
 
Tume iliyoteuliwa na mtuhumiwa, na isiyoakisi jamii ya watanzania sio tume huru wala shirikishi.
  • Mwakilishi wa GenZ yuko wapi?
  • Mwakilishi wa mawazo mbadala yuko wapi?
  • Mwakilishi wa wanaosimamia ukweli na haki, taasisi za kiimani wako wapi?
Utapeli mtupu. Hadi kwenye maafa. Hii sio Serikali ya wananchi.
Naunga mkono

Ila hawa wapuuzi awatoi nafasi ya kuuliza maswali kama wanatoa basi hao wauliza maswali wamepangwa na wanasoma script tu, wanapenda kusikilizwa wao tu
 
Back
Top Bottom