Waziri Mkuu: Tumesikia mijadala, hofu kuhusu makubaliano ya Bandari. Tumeanza kutoa elimu ya kuwapa faraja Watanzania

Waziri Mkuu: Tumesikia mijadala, hofu kuhusu makubaliano ya Bandari. Tumeanza kutoa elimu ya kuwapa faraja Watanzania

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa amekiri kuwa ni kweli tangu Bunge la Tanzania liliporidhia azimio la Nchi ya Tanzania kuimarisha mahusiano yake Nchi ya Tanzania na Nchi ya Dubai hasa katika maeneo ya Kiuchumi na Kijamii, kumekuwa na mijadala mingi, maoni, ushauri na hofu za Uwekezaji nchini

Amesema “Nataka niwahakikishie Serikali yenu makini tumesikia hili na tunaendelea kufuatilia mijadala hiyo na hasa zile hofu na kwa kweli tumeanza kutoa elimu za kuwapa faraja Watanzania”
 
Professional liar at work 😂
IMG_0730.jpeg
 
Professional liar at work 😂

"RAIS MAGUFULI YUKO SALAMA NA ANAENDELEA KUCHAPA KAZI KAMA KAWAIDA." alisema kwa umaridadi wa sauti, Akaendelea kufafanua "Unataka Rais aonekane Kariakoo anazurura?, huko sio mahala pake, mahala pake ni Ikulu, Watanzania tuwabeze wanaoliombea mabaya Taifa letu" alimaliza huku akinyoosha kidole na kukemea vikali wanaotaka kupiga maombi kuombea Afya ya Kiongozi wao JPM!
 
.
Watanzania hatuhitaji kufarijiwa sisi sio watoto. Na wala hatukatai uwekezaji, tunalalamikia vipengele vibovu vya mkataba. Walishughulikie hilo kwanza sio kupiga bla blaa.
.
Halafu huyu alisema jiwe mzima na anaendelea vizuri na majukumu yake kumbe......Uaminifu ni kama bikira ya mwanamke, ikitoka imetoka haiwezi kurudi. Huyu jamaa hatuna imani nae.
 
Amesema “Nataka niwahakikishie Serikali yenu makini tumesikia hili na tunaendelea kufuatilia mijadala hiyo na hasa zile hofu na kwa kweli tumeanza kutoa elimu za kuwapa faraja Watanzania”
Huyu waziri mkuu mzima kweli? Yaani majibu ya ubovu wa mkataba wa DP World ni elimu ya faraja kwa wananchi?
 
Majaliwa Majaliwa Kassimu

Nimekuelewa Kiongozi
 
Ona kauli wanazotoa viongozi wetu!! Eti tunatoa elimu ya kuwapa faraja watanzania!! Kwa hiyo amekubali kuwa huo mkataba ni wamaumivu?!
 
Back
Top Bottom