Waziri Mkuu tunaomba watu wa Kipunguni walipwe pesa zao, Wananchi wanaibiwa, kesi za malalamiko zimejaa Stakishari

Waziri Mkuu tunaomba watu wa Kipunguni walipwe pesa zao, Wananchi wanaibiwa, kesi za malalamiko zimejaa Stakishari

Pdidy

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
62,101
Reaction score
38,487
Mh. Waziri Mkuu wa Tanzania,
Waziri wa Ujenzi,
Waziri wa Ardhi husika,

Naomba niwaombe wananchi wa Kipunguni walipwe fidia zao, jamani.

Mmeondoa baadhi ya watu, lakini sehemu zilizobaki sasa zimegeuka maeneo ya uchimbaji mchanga. Usiku, baadhi ya watu hugeuka majambazi.

Kesi za malalamiko zimejaa stakishari. Tumeenda TAA kulilia suala la malipo, lakini hakuna kinachoendelea.

Hivi sasa watu wanaibiwa hata mchana. Usiku ukirudi Kipunguni, unatembea na Biblia; wakikukaba unawaambia ulipotoka.

Kwa kweli wananchi tunateseka sana. Tunataka kuondoka, na tumekubali kuondoka. Kwa nini tunateseka hivi?

Hivi majuzi baadhi ya wanawake na watoto wadogo wameanza kubakwa.

Kwa kweli inasikitisha sana. Wananchi hawajapinga kuondoka, lakini sasa ni takribani miaka mitatu bado hatujaondoka. Wengine wameondolewa, wengine wamebaki na mateso.

Hivi sasa hata wazee wameanza kufa bila kupata fedha zao. Hili si jambo jema kwa taifa.

Mwisho, tunaomba tupate muda wa kuonana na wananchi wa Kipunguni ili wakueleze ukweli wa kinachoendelea.

Tumeunda kamati zaidi ya tano. Kila anayekwenda huambiwa "njoo kesho" na TAA, na mwisho hujitoa.

Tunaomba, baba, chini ya miguu yako, tulipwe ili tuondoke kabisa katika eneo hilo.

Mungu awabariki wana Kipunguni.

Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
 
Back
Top Bottom