Waziri Mkuu wa Bangladesh, Sheikh Hasina ajiuzulu kutokana na maandamano Yanayoendelea

Waziri Mkuu wa Bangladesh, Sheikh Hasina ajiuzulu kutokana na maandamano Yanayoendelea

Kakimbilia India,lakini katafuna sana miaka ishirini madarakani si haba.
 
Nadhani maelezo sahihi ni kafurumushwa.

Hajajiuzulu kwa hiari yake.

Leo waandamanaji walikuwa wamepanga kwenda kwenye ikulu yao ili wakamtoe kwa nguvu.

Ndo naye akaamua kukimbia nchi.
 
Bi Sheikh Hasina amejiuzulu kufuatia Wimbi la Waandamanaji Vijana (Gen Z) lililoanzishwa na Vijana wa Vyuo Vikuu ambao walikuwa wanalalmika kukosoa mfumo unaowapa kazi Watoto wa Vigogo waliopambania uhuru na kuwatenga Watoto wa maskini.

Bi Hasina ambae ametoka kushinda uchaguzi miaka 2 iliyopita amelazimika kujiuzulu licha ya vikosi vya usalama kupambana na waandamanaji lakini havikufaulu kuwarudisha nyuma ambapo zaidi ya watu 150 waliuwawa kwenye maandamano hayo.Ameondoka Nchini humo kwenda kuishi India.

View: https://www.instagram.com/p/C-SL0oMqVg1/?igsh=MXdkdmhkazI4YnM1NQ==

My Take
Kuzuia watu mil.170 sio rahisi,ndio maana Rais msikivu Dkt.Samia aliwatolea uvivu wazalishaji wa Sukari na chakula kwamba bei za vitu hivyo zisipande maana Gen Z hawaeleweki ,wanaweza liamsha.

View: https://twitter.com/MwanzoTvPlus/status/1820404606096048622?t=8x3bUC89ukBd7_I0HrMyWA&s=19

Pia soma Kuelekea 2025 - Rais Samia: Bei ya Sukari Ikiwa Juu Gen Z Wataingia Barabarani

Sheikh Hasina Wazedhttps://en.m.wikipedia.org/wiki/Sheikh_Hasina#cite_note-3 (born 28 September 1947) is a Bangladeshi politician[2] who served as the tenth prime minister of Bangladesh from June 1996 to July 2001 and later from January 2009 to 5th August 2024. She is the daughter of Sheikh Mujibur Rahman, the founding father and first president of Bangladesh. Having served for a combined total of over 20 years, she is the longest serving prime minister in the history of Bangladesh. Before leaving office in 2024, she was the world's longest-serving female head of government.[3]
 
Vuguvugu lilianza miezi 9 iliyopita yaani November 2023

View: https://m.youtube.com/watch?v=X9en6WDBDso

Nini kinatokea Bangladesh? Watu wametoka barabarani wakimtaka Waziri Mkuu Sheikha Hasina ajiuzulu. Wiki iliyopita, kiongozi wao mkuu wa Upinzani Mirza Fakhrul Islam Alamgir alizuiliwa baada ya maandamano kuwa ghasia. Nini kinasababisha machafuko haya na watu wamepoteza imani na waziri mkuu wao?
 
Matatizo ya ajira na mfumuko wa bei uliopindukia yataichafua sana dunia kwa siku nyingi zijazo. Watawala wengi hawana solutions za maana kuhusu haya mambo.
 
Bi Sheikh Hasina amejiuzulu kufuatia Wimbi la Waandamanaji Vijana (Gen Z) lililoanzishwa na Vijana wa Vyuo Vikuu ambao walikuwa wanalalmika kukosoa mfumo unaowapa kazi Watoto wa Vigogo waliopambania uhuru na kuwatenga Watoto wa maskini.

Bi Hasina ambae ametoka kushinda uchaguzi miaka 2 iliyopita amelazimika kujiuzulu licha ya vikosi vya usalama kupambana na waandamanaji lakini havikufaulu kuwarudisha nyuma ambapo zaidi ya watu 150 waliuwawa kwenye maandamano hayo.Ameondoka Nchini humo kwenda kuishi India.

----
Waandamanaji vijana wamekuwa wakiimba wakimtaka waziri mkuu wao aondoke madarakani.

Bi Hasina mwenye umri wa miaka 76 ametawala taifa hilo la Asia Kusini lenye watu milioni 170 kwa mkono wa chuma tangu 2009.

Miaka yake 15 madarakani imejawa na shutuma za kutoweka kwa watu, mauaji ya nje ya mahakama, na kukandamizwa kwa watu wa upinzani na wakosoaji wake na anakanusha mashtaka,

Pia soma Kuelekea 2025 - Rais Samia: Bei ya Sukari Ikiwa Juu Gen Z Wataingia Barabarani
Pigia mstari KUTOWEKA KWA WATU.
 
Back
Top Bottom