Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson aamua Lockdown sasa basi

Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson aamua Lockdown sasa basi

Tutaelewana tu! Watanzania tupige Kazi!

Mlisha mshauri raisi kipindi ugonjwa haujaingia kuwa asifanye lockdown na raisi akasikiliza ushauri wenu hakufunga mipaka wala hakufanya lockdown kwa jiji la Dar sasa mnahangaikana nini

Maana kwa sasa lockdown kwa Tanzania haiwezekani tena ugonjwa umeshafika kila sehemu hadi katika mapapai na mbuzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kwa akili zenu nchi zililock milele ?Kila Kiongozi akifungua nchi basi kamuiga Magufuli. Huyo Boris hata Magufuli hamjui kabisa.
Hakuna rais duniani kwasasa ambaye hajasikia jina la Magufuli katika kipindi hiki cha Corona, Magufuli ni gumzo la dunia nzima kwa sasa kutokana na utofauti anaoutumia katika kupambana na Corona.

Muhimu sio kumjua au kutomjia, kile kitendo cha Boris na marais wengi kuchukua maamuzi ambayo mwanzilishi wake ni Magufuli, inaonyesha uwezo mkubwa alionao Magufuli ktk kuona mbali, kwamba hapelekeshwi hovyo na misimamo ya duniani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanafungua nchi kwa sababu sasa wameshajua jinsi ya kudeal na wagonjwa,hospital zao wameziwezesha kuja kuweza kupokea wagonjwa. Na curve imeanza ku flatten.
Kwa Akili zenu Beberu akirudi kazini mnafikiria eti ni wamachinga wao wanarudi barabarani? Beberu amerudi afrika kuchimba madini, - Miafrika muendelee kujifungia huku mkisherehekea mikopo
 
Imefika muda ma Rais wa Mataifa Makubwa wajue kuna Akili kubwa a.k.a Darubini a.k.a kiona Mbali anaitwa Dr John Joseph Pombe Magufuli

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi slogan ya "Chukuwa Tahadhari " ndio slogan ya Magu? Bora kunywa mkojo wa mbwa kuliko mkojo wa uzwazwa.


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Mwambie aje dar tuchape kazi sio anajificha huko kijijini.
Ikumbukwe duniani kote ni JPM tu ndie alieasisi precaution hii ya chapa kazi lakini chukua tahadhari

Alionekana kituko dunia nzima mpaka chang'aa media ya kunyaland kuja na slogan ya ukaidi wa Magufuli, baada ya kuonja shubiri ya kuomba msamaha week nzima,

Chang'aa media hiyo iliajiri watu mitandaoni kumtukana na kumkashifu JPM

Nangoja hash tag ya ukaidi wa Borris mungu wao

20200510_234631.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ugonjwa umeisha baada ya lockdown?
Maambukizi yameisha au kupungua au yamepaa?
Elimu juu ya kujikinga imeeleweka miongoni mwa jamii?

Kuna mengi ya kujifunza na kuyafanyia kazi.

Hivi kwa akili zenu nchi zililock milele ?Kila Kiongozi akifungua nchi basi kamuiga Magufuli. Huyo Boris hata Magufuli hamjui kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania kweli mnakasoro......hahaa. Most European countries are now easing lockdown measures since the rate of new infections has reduced. Halafu the easing of lockdown is gradual si ati wanaamka leo na kurudia hali ya kawaida....hahaa
 
Wanafungua nchi kwa sababu sasa wameshajua jinsi ya kudeal na wagonjwa,hospital zao wameziwezesha kuja kuweza kupokea wagonjwa. Na curve imeanza ku flatten.
Hapa kwetu kiongozi hajaridhia hatua za nchi zingine
Jihadhari, ugonjwa upo, chapa kazi, omba Mungu, fukiza nyungu, tumia tiba mbadala, shule na vyuo vimefungwa, updates hazitolewi tena.
Sio lazima kuigana kila kitu, ugonjwa haujapata dawa bado, tuendelee na maisha tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wale walifunga wanafungua, wewe hujafunga unatakaje kufanana nao!!??
Hakuna kilichobadirika kwao na hata kwenye nchi ambazo hazikufunga hakuna uogofyo Wala nini

Wamewaumiza wanachi bule kuwafungie na nchi zingine inabidi watawala Wao wafikishwe mahakamani haraka Sana baada ya kuamuru mapolice kuwauwa ambao walikuwa wakitoka nje baada ya kuwafungia

Swali la kujiuliza, Kwa nini wanaondoa Sheria ya kuwafungia watu Wakati Hali ya maambukizi ikiendelea na ugonjwa hauna hata Dalili ya kuondoka?

Hongera Raisi wangu, najua siwezi kukutana na wewe kukupa shakrani zangu zikiambatana na Watanzania wengi Sana na wengine Kwa sababu tu ya kutimiza misimamo ya viongozi wao lakini wakiwa mbali na viongozi wao wanaungana na Watanzania wengi kukupa hongera, Basi Kwa pamoja pokea shukrani zetu kupitia jukwaa letu pendwa kabisa La JF, Mungu akubariki sana, umenisaidia Mimi binafs sababu naendelea kujipatia vijisenti vya kukizi mahitaji yangu na watoto wangu...kama ungefunga, ningekuwa natokwa na matusi makubwamakubwa ya kulaani huku nikifa Mimi na watoto wangu kidogokidogo huku najiona,
 
Watanzania kweli mnakasoro......hahaa.Most European countries are now easing lockdown measures since the rate of new infections has reduced.Alafu the easing of lockdown is gradual si ati wanaamka leo na kurudia hali ya kawaida....hahaa
Je UK na USA rate of new infections and deaths have reduced?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kufungia watu ndani wakati ugonjwa haufahamiki unaisha lini ni uzwazwa wa ajabu sana,

Ni mwendo wa kujifunza kukabiliana na kuishi na hili gonjwa maana hakuna namna sasa.

Kule UG wananchi wameanza kula panya kutokana na kukosa chakula.
 
Swali la kujiuliza, Kwa nini wanaondoa Sheria ya kuwafungia watu Wakati Hali ya maambukizi ikiendelea na ugonjwa hauna hata Dalili ya kuondoka?
Hii hoja si sahihi hata kidogo. Mnaodhani kwamba "lock down" haijawasadia hao watu wa Ulaya mnakosea sana na wala siyo kweli kwamba "Lock down" inaondolewa kwa sababu imeshindwa kufanya kazi.

Ulaya Maambukizi yanapungua sana kuliko mnavyotaka kuaminisha watu. Wao wanapima watu wao, wanaweka ufuatiliaji, wanafanya tathimini za kisayansi kuhusu COVID 19 na hali ya uchumi ilivyo.

Hakuna mtu yeyote mwenye akili timamu aliyedhani kwamba "Lock down" litakuwa ni jambo la milele. Sielewi ni kwa nini kuna baadhi ya watu wanashangaa kuona baadhi ya mashart ya "Lock Down" yanapunguzwa huko Ulaya na Marekani!!
 
Back
Top Bottom