Waziri mkuu wa Urusi Dmitry Medvedev amewasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa rais


Si kweli kwamba Medvedev kipindi akiwa rais alikuwa sio mkuu wa nchi, HAPANA. Medvedev alikuwa ni bosi wa Putin kama vile tu sasa Putin alivyo bosi wa Medvedev. Medvedev alikuwa rais, mkuu wa nchi, mkuu wa serikali na amir jeshi mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Waziri mkuu wa Urusi Dmitry Medvedev amewasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa rais Vladmir Putin leo.

Putin alikutana na Medvedev baada ya rais kutoa hotuba yake kupitia televisheni ya taifa ambamo amependekeza kufanyia mageuzi katiba ili kulipa bunge uwezo wa kumteua waziri mkuu.

Kwa hivi sasa rais ana mamlaka ya kumteua waziri mkuu. Medvedev alinukuliwa akisema kuwa katika muktadha huu ni wazi kwamba , baraza la mawaziri , linapaswa kumpatia rais wa nchi hiyo fursa ya kuchukua hatua zote zinazostahili.

Putin alinukuliwa akimuelekeza Medvedev kuendelea kuwa katika wadhifa wa waziri mkuu hadi pale baraza jipya la mawaziri litakapoundwa.

Putin alisema katika hotuba yake kwa taifa kuwa Medvedev atateuliwa kuwa naibu mkuu wa baraza la taifa la usalama nchini humo. Putin ni mkuu wa baraza hilo.
 
2008-2012....Putin aliamua kuweka madarakani kama Rais , ili kutoa nafasi yake tena yakua Rais ...


Ndo maana 2012 ..Putin akarudi kua Rais, na Medvedev akarudi kua Waziri mkuu

Putin yupo kwa Urais toka 1999/1/31


Kama umefatilia Speech yake kwa Feds ,Jamaa anatengeneza mazingira yakuendelea kuiendesha Russia hata baada ya muda wake kuisha 2024 , ndo maana Medvedev kajiuzuru.
 
Ni kweli Medvedev alikuwa ndiye mkuu wa nchi, ila kumbuka vizuri au fanya marejeo ya taarifa uone kilichofanyika kabla Medvedev hajawa rais na Putin kuwa Waziri mkuu. Kati ya masharti ilikuwa ni kuhakikisha kwamba akishashinda urais anamteua Putin kuwa Wazuri mkuu.

Ilikuwa kama ilivyokuwa kipindi kile Kagame alipokuwa makamu wa raus Rwanda.

Putin anafanya usanii sana ili aendelee kuwa Powefulman
 
... hivi hakuna warusi wengine wenye sifa kuongoza taifa lao? Kwa kupenda madaraka huyu hana tofauti na madikteta ya kiafrika.
 
Kama umefatilia Speech yake kwa Feds ,Jamaa anatengeneza mazingira yakuendelea kuiendesha Russia hata baada ya muda wake kuisha 2024 , ndo maana Medvedev kajiuzuru.
Siyo kwamba anaimarisha maamuzi ya kidemokrasia nchi Russia, kweli? Kulipa nguvu bunge kwa kupunguza madaraka ya rais wakati huo huo ukiimarisha nafasi ya waziri Mkuu kuna ubaya gani kidemokrasia! Tatizo kila west ikianzisha mchezo inajikuta imepigwa kwenye mchezo huo huo iliouanzisha!! West walisema Russia kuna mapungufu ya demokrasia ...sasa Putin katia mguu mazima kushamirisha demokrasia, west wanaibuka eti Putin anajiandaa kuendelea ku'shikilia' madaraka ya nchi! Beaten on their own game of Democracy, h ah aaha aa!
===
Kwa kukukumbusha tu D.Medved amepewa nafasi ya makamu mwenyekiti wa Balaza la Usalama la Russia (chombo muhimu na kikubwa sana nchini humo) ambacho ni Rais pekee alikuwa mwenyekiti bila msaidizi. Unganisha dots... !
 
Putini anataka kuwa Waziri Mkuu mwenye nguvu kuanzia 2024, nachokiona Russia hawaaminiani wale ambao wako katika baraza la Usalama la nchi, wameshindwa kumpata Mrithi/ Mbadala wa Putini kwa maana hiyo Putini ni Russia hadi atakapofariki
 
Putin anacheza na katiba ya nchi yake ili ajihakikishie nafasi ya kubakia Kremlin miaka ijayo.
 
Putini anataka kuwa Waziri Mkuu mwenye nguvu kuanzia 2024, nachokiona Russia hawaaminiani wale ambao wako katika baraza la Usalama la nchi, wameshindwa kumpata Mrithi/ Mbadala wa Putini kwa maana hiyo Putini ni Russia hadi atakapofariki
Yani nikisomaga habari za hawa watu wawili nabaki nacheka tu.
Ndio maana Russia hawahangaiki na kitu kinachoitwa Democracy kwa kuwa wao hawana kabisa
 
Kama Uwepo wake madarakani katika ikulu ya Kremlin unatija ' ' Na Bado unatoa Upinzani mkubwa kwa mataifa Adui ya Russia ....huku akiendelea kuifanya Russia kuwa nchi kubwa na Yenye ushawishi Duniani ....Basi aendelee tu kuwepo madarakani mpaka Kufa kwake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu Putin huwa anaifanya Russia kama kaiumba yeye anageiuza geuza kama anakaanga samaki kwa jinsi anavyofikiri na huyu Medvedev kila anachopangiwa kwake hewala bwana mkubwa, akiambiwa utakuwa rais sawa, utakuwa waziri mkuu sawa utakuwa katibu wa usalama kwake hewala ili mradi mambo yake yanakwenda
 
Ndo maana nakuambia Putin mjanja... Hilo baraza ,yeye mwenyewe ndo kalianzisha.

Medvedev kua Makamo maana yake kuna Mkuu wake...

Mkuu wake niyupi??? Atakua Putin mwenyewe.

Putin mazingira haya...

Kwanza anaweza kuchaguliwa na Bunge kua Waziri Mkuu ndio maana unaona anakupa bunge mamlaka + kumpa Waziri Mkuu mamlaka.


Au kupitia hili Baraza, ambapo yeye atakua Mkuu ,na Medvedev kua Makamo wake...( kumbuka ili baraza ndio kitakua linaongoza masuala muhimu yote ya kitaifa ikiwemo Ulinzi na usalama na uchumi ,HAPA JAMAA ANATAKA KUA KAMA AYATOLLAH WA IRAN)....


Kumpunguzia Rais madaraka ni anajaribu kuibadili Urusi kua kma Iran..


NB..Putin alikua anauwezo wa kufanya kama Xi jinping , Ila ye kaamua kutumia njia nyingine ..

Mwamba anaamini Urusi inamuhitaji sana, ndio sababu hata wakat kampan Medvedev Urais, BADO YEYE NDO ALIAMUA KILA KITU NAHATA MAJESHI NA VYOMBO VYA USALAMA VILIKUA VINAFUATA MAAGIZO YAKE KULIKO YA Medvedev .......pitia vita ya Russo- Georgian war .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…