Katiba ya Urusi inasema rais atatawala kwa vipindi viwili kama atachaguliwa, haisemi kama inamkataza baada hivyo vipindi viwili akakaa pembeni halafu akarudi tena kugombea
Hivyo Putin alitumia loophole hiyo ya katiba kutosema chochote kumlataza rais anayemaliza vipindi vyake viwili akakaa pembeni na baadaye kurudi tena kugombea.
Kipindi kile akamuandaa Dmitry Medvedev kuwa rais lakini kabla akahamishia nguvu na mamlaka kubwa kwa waziri mkuu halafu yeye akaenda kuwa Waziri mkuu halafu Dmitry Medvedev akawa rais lakini asiye na nguvu, hata wakuu wa nchini walipotaka kukutana na mkuu wa nchi ya Russia, walikutana na Waziri mkuu Putin.
Wakati Dmitry Medvedev anaelekea ukjngoni mwa utawala wake, Putin akaenda tena Bungeni kuhamisha madaraka kutoka kwa waziri kwenda kaa rais akijua atashinda tu.
Hivyo anachokifanya hivi sasa ni marudio tu na binafsi nilikitarajia sana.
NDIYO MAANA NIKASEMA PUTIN HAIVUNJI KATIBA BALI ANAIPIGA CHENGA.