Carlos The Jackal
JF-Expert Member
- Feb 6, 2017
- 25,725
- 78,589
Kuna uwezekano Putin akawa waziri mkuu 2024 na kuendelea kuwepo.
Putin ilo analijua sana... Sasa mwendo niyeye kuwepo tu ..Putini anataka kuwa Waziri Mkuu mwenye nguvu kuanzia 2024, nachokiona Russia hawaaminiani wale ambao wako katika baraza la Usalama la nchi, wameshindwa kumpata Mrithi/ Mbadala wa Putini kwa maana hiyo Putini ni Russia hadi atakapofariki
ukiangalia hesabu za wamagharibi ilikua nikuhakikisha wanaisambaratisha Urusi kupitia mapandikizi kama ulivokua kwa Mikhail Ghobachev alivyoivunjavunja USSR ..Putin ilo analijua sana... Sasa mwendo niyeye kuwepo tu ..
Nkm hapa bongo kwetu, Jinsi JIWE atakavyofanya mambo yake
Hahahaha, inawezekana sana tu ,upepo ushapita ,twende 2023 tuoneDuh! Ina maana Jose huenda akarudi ikulu tena?..[emoji849][emoji849]
Joseph Kabila na yeye alichofanya ni kuipiga chenga Katiba. Ndiyo maana kajenga ushawishi na kuwekeza nguvu kwenye Chama na Chama kimelikamata bunge.Hizo mbinu naona na ndugu yangu Jose anataka kuzitumia
MTC | 101| [emoji769]
Hahahaha, salute kwako Mkuu kwa kuliona hili , 2023Joseph Kabila na yete alichifanya ni kuipiga chenga Katiba. Ndiyo maana kajenga ushawishi na kuwekeza nguvu kwenye Chama na Chama kimelikamata bunge.
Anataka Rais ajae asiwe na mamlaka makubwa bali nguvu zaidi awe nayo Waziri Mkuu ni hilo tu
Naona anataka kumuweka mtu wake kama PM
Sent from my iPhone using Tapatalk
Maishani tafuta mshikaji wa kufaana kama Vladimir na Dimitri
Katiba ya Urusi inasema rais atatawala kwa vipindi viwili kama atachaguliwa, haisemi kama inamkataza baada hivyo vipindi viwili akakaa pembeni halafu akarudi tena kugombea
Hivyo Putin alitumia loophole hiyo ya katiba kutosema chochote kumlataza rais anayemaliza vipindi vyake viwili akakaa pembeni na baadaye kurudi tena kugombea.
Kipindi kile akamuandaa Dmitry Medvedev kuwa rais lakini kabla akahamishia nguvu na mamlaka kubwa kwa waziri mkuu halafu yeye akaenda kuwa Waziri mkuu halafu Dmitry Medvedev akawa rais lakini asiye na nguvu, hata wakuu wa nchini walipotaka kukutana na mkuu wa nchi ya Russia, walikutana na Waziri mkuu Putin.
Wakati Dmitry Medvedev anaelekea ukjngoni mwa utawala wake, Putin akaenda tena Bungeni kuhamisha madaraka kutoka kwa waziri kwenda kaa rais akijua atashinda tu.
Hivyo anachokifanya hivi sasa ni marudio tu na binafsi nilikitarajia sana.
NDIYO MAANA NIKASEMA PUTIN HAIVUNJI KATIBA BALI ANAIPIGA CHENGA.
Umetoa uchambuzi mzuri sana. Shida ya serikali ya Urusi sioni kama ina juhudi sana za kukuza uchumi. Wanapiga kazi sana lakini bado.
Huyu Putin huwa anaifanya Russia kama kaiumba yeye anageiuza geuza kama anakaanga samaki kwa jinsi anavyofikiri na huyu Medvedev kila anachopangiwa kwake hewala bwana mkubwa, akiambiwa utakuwa rais sawa, utakuwa waziri mkuu sawa utakuwa katibu wa usalama kwake hewala ili mradi mambo yake yanakwenda
Uwekezaji katika ulinzi ni muhimu kwao. Bila hivo wangekuwa hawapo tungebaki na stori kama ya Yugoslavia. Ikitokea wakaona umuhimu zaidi wa private sector na innovation watapiga hatua kubwa zaidi. Then ikitokea mafuta yakapanda hizo fedha za ziada najua sahivi wataziwekeza vizuri zaidi.Wanajitadi,sema tu vikwazo vya US na uwekezaji mkubwa kwenye masuala ya ulinzi. Kumbuka,kila wakati Urusi lazima waendelee kuwa kitisho kwa NATO ili awe salama.
Sent using Jamii Forums mobile app
Naaam hakika.........Kama Uwepo wake madarakani katika ikulu ya Kremlin unatija ' ' Na Bado unatoa Upinzani mkubwa kwa mataifa Adui ya Russia ....huku akiendelea kuifanya Russia kuwa nchi kubwa na Yenye ushawishi Duniani ....Basi aendelee tu kuwepo madarakani mpaka Kufa kwake
Sent using Jamii Forums mobile app
Hana tofauti na mbowe ,,,anaminisha watu akiingia mwingine atakuwa kibaraka was America... hivi hakuna warusi wengine wenye sifa kuongoza taifa lao? Kwa kupenda madaraka huyu hana tofauti na madikteta ya kiafrika.