Waziri mpya wa Mawasiliano, anza kazi na Azam Media. Wamepanga kutupiga kwenye vifurushi vipya

Waziri mpya wa Mawasiliano, anza kazi na Azam Media. Wamepanga kutupiga kwenye vifurushi vipya

Ndugu Mteja, kuanzia 1/8/24 kutakuwa na mabadiliko ya bei. Kifurushi cha 25000 kuwa 28000; 17000 kuwa 19000; 10000 kuwa 12000; 6000 kuwa 7000 na 3000 kuwa 4000.

Azam decoder hawana Ubora kuzidi Dstv, Wanatumia kigezo cha kutuonyesha mipira Ili kuchaji gharama zaidi, ongezeko hilo ni kama blackmailing, hakuna media nyingine wanaowapa ushindani kwenye mpira kwa Sasa. Ongezeko hilo sio halisia na maisha ya wananchi, ajabu Mzawa mwenzetu anatunyonya kuliko wageni wawekezaji.

Mmesubiri home boy apigwe chini ndio mlete ongezeko! Waziri nakusihi, liangalie kwa jicho la wananchi wanyonge..
Wamenitumia ujumbe ni wahuni sn, sababu za kupandisha ni nini?
 
Halafu nasikia wenzetu wa nchi jirani, bei ya vifurushi iko chini kuliko hapa kwetu!! Sasa sijui shida iko wapi!!
 
Huwa nashangaa quality ya rangi ya Azam, tofauti kabisa na Dstv, and i was told kwamba kadri quality inavyokuwa kubwa, ndivyo gharama zinaongezeka(niliambiwa kwenye kijiwe cha kahawa).

Anyway, tumeshangilia yale mavifaa ya Azam Tv, sijui kamera ya milioni 500 na kumsifia Azam kwamba ni tajiri, kumbe sisi tumeyanunua kwa tozo hizo za vingamuzi
Kwahiyo ulikuwa unataka kwa bei ileile?
 
Kwani Azam wanapata ruzuku serikalini? Hii ni biashara ya mtu binafsi na mfanya biashara yoyote lengo ni faida. Haya mambo hayamuhusu waziri wala serikali ni maamuzi ya kampuni binafsi hata sokoni tunaenda tunakutana na bei mpya lakini tunanunua. Kwa Azam kama huliwezi ni kuhamia sehemu unayoweza hakuna aliyelazimishwa kununua.
Lazima kuwe na control, mabasi ya Shabiby, Ngasere, Mtei yanapta ruzuku? mbona nauli inapangwa na LATRA? kuwa na akili kidogo
 
Upo sawa kichwani kweli? Leo ukiuziwa saruji 100000 mfuko1 kwakuwa ni biashara ya mtu utaona ni Sawa? Nyie ndiyo majinga mliopo nchini. Serikali kazi yake ni ku regulate na ku control inflation ili wananchi wapate huduma kwa bei nafuu.
Muwe mnaelewa huduma mnazozitaka azam TV zinatoka nje ya nchi yeye anauziwa kwa bei ya juu sasa na nyie mnataka muuziwe kwa bei ya chini bado serikali itoze kodi hivi hapa kutakua na biashara au upuuzi? Itumeni serikali yenu ikaombe huko ulaya na marekani azam apunguziwe bei ili msilipie hela nyingi na kodi huyo azam asamehewe asilipe .
 
Upo sawa kichwani kweli? Leo ukiuziwa saruji 100000 mfuko1 kwakuwa ni biashara ya mtu utaona ni Sawa? Nyie ndiyo majinga mliopo nchini. Serikali kazi yake ni ku regulate na ku control inflation ili wananchi wapate huduma kwa bei nafuu.
Hebu mweleze huyu naye. Lazima kuwe na bei elekezi kwani hata hao azam kuna vitu vingi wanapata toka serikalini katafute mambo ya uwekezaji uone. Pili hata urushaji wa matangazo yao kuna frequency ambazo wamepewa na serikali. Azam kama pesa anazipata sana na jeuri hii inakuja baada ya kuona yupo pekee ambaye watu wengi wanatumia service yake kuanzia mpira mpaka zile movie za kibongo,uturuki na kikorea. Ila anachokifanya siyo sawa kabisa maana hata kodi sijaona wapi wameongeza. Nadhani ni wakati sasa wa serikali kumpa nafuu DSTV ili ushindani uwe fair maana jamaa azam anapata favour kama mzawa lakini garama anafukuzana karibu sawa na dstv. Huu ni wizi kwa wananchi kila wakati kuongeza garama pasipo kuwa na sababu zozote za msingi.
 
Azam waje hapa kutoa ufafuzi,wasidhani kuonesha Ligi kuu Bara na kuja na VAR ndio Kihalalisho Cha kutupiga kwenye bei za Vifurushi Vyao kuanzia 1/8/2024.

Waziri wa Mawasiliano Anza na Hili.View attachment 3050740
Wanaonesha La liga , serie A , Bundslesliga , France , baadhi ya match za Epl , afcon na ligi kibao bado mnataka kwa elfu 20 hivi watanzania nani kawaroga ? Na hapo ni full HD aah bana acheni hizo.
 
Azam wapo sahihi kupandisha bei, Mara nyingi inshu ya kodi anayeumia ni mlaji wa mwisho
 
Azam waje hapa kutoa ufafuzi,wasidhani kuonesha Ligi kuu Bara na kuja na VAR ndio Kihalalisho Cha kutupiga kwenye bei za Vifurushi Vyao kuanzia 1/8/2024.

Waziri wa Mawasiliano Anza na Hili.View attachment 3050740
Wanaonesha La liga , serie A , Bundslesliga , France , baadhi ya match za Epl , afcon na ligi kibao bado mnataka kwa elfu 20 hivi watanzania nani kawaroga ? Na hapo ni full HD aah bana acheni hizo.
 
Waziri mpya wa habari awanyang'anye Azam TV hiyo monopoly ya mpira. TBC, ITV, Star TV, Clouds TV, Channel Ten, EATV etc nao waruhusiwe kuonesha hizo live football matches. Hapo lazima vifurushi vya Azam TV vitashuka automatically na jeuri hii ya Azam TV itakoma.
Unajiita Dr Akili lkn Mm nakuambia hv, ww huna akili.

Hao wote uliowaandika hapo kasoro TBC anayelipwa na serikali hao wngn wote ht kulipana mishahara yao wnyw wanashikana mashati ndio waje waweze kuonyesha mechi?
Unajua gharama za kuonyesha mechi au unaongea tuu?

Mwisho wa msimu Azam anatoa 900m+ kwa timu zote na hapo bado anatakiwa kutoa pesa kila mwezi kwa kila timu, haya nambie n Tv station Gani kati ya hizo ulizotaja zinaweza kutoa hy pesa wakati mishahara yao tuu hawawezi kulipana.
 
Hata kama million nalipia tu ila quality na vipindi vinaeleweka sio ao azam matapeli channel kama ukungu vipindi. Vya watu wa buza tu Mpira wa wavunja kuni wa tanzania yaani Mimi niangalie uchafu wa ligi ya tanzania
Wewe kalipie huko kwa milioni sisi wengine uwezo hatuna tutabaki azam kwa bei nafuu
 
Wanaonesha La liga , serie A , Bundslesliga , France , baadhi ya match za Epl , afcon na ligi kibao bado mnataka kwa elfu 20 hivi watanzania nani kawaroga ? Na hapo ni full HD aah bana acheni hizo.
Wazitoe zote hizo wabakize za Bongo tuu na bei irudi ilikokuwa.

Hii ni Nchi ya wanyonge 😂😂😂😂
 
Lazima kuwe na control, mabasi ya Shabiby, Ngasere, Mtei yanapta ruzuku? mbona nauli inapangwa na LATRA? kuwa na akili kidogo
Sababu bei ya mafuta inapangwa na serikali. Ok sasa kwanini wasipange bei za ndege? za hotel? za nyama? wewe umeona mfano Shabiby tu. Kwa hiyo ma bus yote ni bei moja? unaweza kupanda Shabiby la alfu 20 liko 25 yako mpaka 40. Hakuna biashara ya kupangiana bei korosho tu mlitia mkono mkauwa. Biashara ni ushindani huwezi Azam hamia DSTV huko huwezi wako kina Startimes sio kupangiana bei. Lete sehemu ilitolewa wapi bei elekezi ya Ving'amuzi.
 
Sukari mbona wamepangiwa? serikali inaagiza sukari? acha ushamba, sasahivi kuna bidhaa muhimu duniani kama information? na ni haki no 1, kama hataki kupangiwa bei arudi kwao uarabuni akafanye biashara huko
 
Back
Top Bottom