Waziri Mwakyembe ' mfowadie ' haraka Bosi wako JPM hizi ' SMS ' za Watanzania kutoka Mitandaoni kwa Kocha Amunike


Hizo sababu zenu mbona hamkuzisema au hamkushauri mapema ili ' advance team ' iliyoenda huko ichukue tahadhari na itusaidie katika Ushindi? Ndiyo maana kila Siku huwa nasema kama kuna Taifa ambalo lina Watu ' Wanafiki ' waliotukuka basi ni Tanzania na kama Waandaji wa Michezo ya Olympic wakiweka Kipengele cha ' Unafiki ' nina uhakika kila Msimu wa Mashindano Tanzania tutabeba ' Medali ' nyingi za Dhahabu.

Tumefungwa ' Kiufundi ' zaidi wa Uwanjani na acheni tuliocheza mpira wa Viwango vyetu na tunaoufuatilia 24/7 tutoe nyongo / hasira zetu. Ukweli utabaki pale pale kuwa Kocha Amunike alitepeta kama siyo kutokota katika Upangaji wa Timu jana na sasa ameanza Kutufanya wengine tuanze Kuhisi kuwa huenda ' alihongwa ' na ama Lesotho wenyewe au hata Cape Verde ili apange Kikosi cha ' Kipopoma ' ili tusifanye vizuri jana.

Acheni kutupandisha hasira zaidi kwa sababu zenu za Kipuuzi / Kipomboyo tafadhalini.
 
Yani wewe akili yako yote ni siasa tu basi!

Dah... Una shida sana wewe
 
Maujanja ya ushindi katika siasa yaende next level Kimataifa! Au ushindi unategemea waamuzi?! Teh
 
Hili neno
 
GENTAMYCINE jana si iliachia mwenyewe hirizi au sio wewe.

Ni kweli niiiachia ' Hirizi ' baada ya ' Mpuuzi ' huyu mbarika ' Kunitibua ' na nilimwambia kuwa naiachia na muda mchache tunafungwa na ndani ya dakika tatu tu tukapigwa ' Kidude ' kilichotung'ang'ania. Na cha Kushangaza huyo huyo mbarika baada ya Kuona kuwa nilichomhakikishia kilitimia akarudi tena Kwangu Kuomba ' po / radhi ' nikamjibu ' Kunya ' na kumwambia kuwa ameshachelewa.

Kuna baadhi ya Watu wanadhani kuwa Mshabiki wa kweli wa Taifa Stars ni mpaka labda usafiri na Timu kokote iendako kumbe wanasahau kwamba kuna Sisi wengine akina GENTAMYCINE michango yetu kwa hii Timu ni hasa katika upande wa Ulozi / Ndumba / Utamaduni / Ushirikina na binafsi nina ' Mtaalam ' wangu huko Pemba Kisiwani Zanzibar ambaye mara zote hakuna ambacho huniambia kinachohusiana na Mpira hasa huu wa Kibongobongo kisitimie.

Siku mbili kabla niliweka Kikosi ambacho Yeye mwenyewe ' Mtaalam ' aliniambia kuwa ndicho kinatakiwa Kianze dhidi ya Lesotho kwakuwa ' Kinyota ' Kingeibeba zaidi Timu na baadae tena baada ya Beki Shomari Kapombe Kuumia akanitumia tena Kingine ambacho kilikuwa na marekebisho machache tu na nakumbuka kila mara alikuwa anasisitiza kuwa kisibadilishwe hadi dakika zote 90 na nikawaomba Watu hapa ' waifowadi ' ile ' Line Up ' kwa Watu wa TFF na Benchi la Ufundi la Taifa Stars nikaonekana kama vile Pomboyo / Mpuuzi fulani hivi na hatimaye jana yametukuta.
 
Mkuu hi thread inmenivunja mbavu ,hivi ikitokea mechi yetu na Uganda tukashinda ,na lethoto wakapoteza


mtampongeza Amunike au ????
 


Mkuu achana na huyu kocha, sijui kala maharage ya aina gani!
 
Kocha hana kosa lolote kwasababu timu ilicheza na ilifanikiwa kufika golini kwa timu pinzani kukakosekana umakini kwasababu tatizo la wachezaji wa nchi hii sio kutokujua kucheza mpira bali matumizi ya akili.Ndo maana kwamuda mrefu sasa hatujawai kufanya vizuri kimataifa.
 
Lesotho ni wepesi sana game plan kwetu ilikuwa very poor hata kikosi kilikuwa dhaifu sana.

Hao hao lesotho walipigwa kwao na UG wakati hawa waganda tuko nao hapahapa bongo
 
Mbona unaongea na kujipinga mwenyewe teteeeteeehh
 
Mkuu hi thread inmenivunja mbavu ,hivi ikitokea mechi yetu na Uganda tukashinda ,na lethoto wakapoteza


mtampongeza Amunike au ????

Sasa kwakuwa mmenichokoza nawawekeeni hapa hapa na matokeo rasmi ya mechi ya Taifa Stars dhidi ya Uganda Cranes na Cape Verde dhidi ya Lesotho na nani atapita kati ya Tanzania, Lesotho na Cape Verde. Na hii ni kwa mujibu wa huyu huyu ' Mtaalam ' wangu hatari wa Kipemba.

Taarifa ikufikie popote pale ulipo ewe Mtanzania kwamba hiyo mechi yetu ya Uganda tutatoka sare ambayo itakuwa ama ya Magoli au isiyo na Magoli ila ni Sare ( Draw ) na mechi kati ya Cape Verde na Lesotho ni kwamba Cape Verde atashinda hivyo Kufikisha alama zake Saba ( 7 ) na kutuacha Tanzania na alama zetu Sita ( 6 ) na Lesotho watabaki na alama zao Tano ( 5 ) na hatimaye Cape Verde ndiyo ataungana rasmi na Uganda kwenda huko AFCON 2019.

Naomba hii ' post ' itunzwe na kila Mtu awe nayo kwani ndiyo ukweli wenyewe na hata Tanzania tufanye nini au tujitahidi kufanya juhudi zozote matokeo ndiyo hayo hayatabadilika. Ushauri wangu tu kwa TFF, Watanzania na hata Rais wetu Dkt. JPM ni kwamba hivi sasa tuwekeze nguvu zetu nyingi kwa Timu za Taifa za Vijana Serengeti Boys na Ngorongoro Heroes ili zifanye vyema katika michuano yao inayoshiriki sasa na pia tuanze sasa Kuiandaa Timu ya Taifa Stars ya Kufuzu na Kucheza AFCON ya 2021 ila hii ya Cameroon mwakani tumeshatepeta kama siyo kutokota na endeleeni tu Kudanganyana na Kupeana moyo.

Nimemaliza.
 
Hilo

Hilo waliliona ndiyo maana timu ilikuwa Bloemfontein (almost same elevation) as well as weather. Wachezaji wenyewe hawana uzalendo hata kidogo tunaweza kumlaumu kocha bure (kama ni mechi ngumu na zenye tension Amunike amezicheza sana,ila Amunike hana sifa za kuwa kocha wa timu za Taifa za wakubwa) .Hopeless,tulivyokuwa tumejipanga kuwapokea leo nchi ingezizima…! Kuna tatizo mahali;mwanzo tulisema walimu wazawa hawana uwezo,tukaleta wazungu hamna kitu tukaleta mwafrika nje ya Tanzania hamna kitu sasa tufanyeje??
 

Kilichobaki ' tutekane ' tu sasa kwani ndicho ambacho tunakiweza kama siyo tunakimudu kwa 100%.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…