GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
- Thread starter
- #21
sodoliki hoja yako ni ya kitaalamu sana unaweza kuiongezea nyama kidogo ili ieleweke? Kuna watu wanadhani kushindwa kupanda Mlima Kilimanjaro ama mlima mwingine ule kunatokana na urefu wake, kumbe mwinuko toka usawa wa bahari huamua uwezo wa mtu kupumua na mwili kutenda kazi ipasavyo ama kama mwili ulivyozoea!!
Hizo sababu zenu mbona hamkuzisema au hamkushauri mapema ili ' advance team ' iliyoenda huko ichukue tahadhari na itusaidie katika Ushindi? Ndiyo maana kila Siku huwa nasema kama kuna Taifa ambalo lina Watu ' Wanafiki ' waliotukuka basi ni Tanzania na kama Waandaji wa Michezo ya Olympic wakiweka Kipengele cha ' Unafiki ' nina uhakika kila Msimu wa Mashindano Tanzania tutabeba ' Medali ' nyingi za Dhahabu.
Tumefungwa ' Kiufundi ' zaidi wa Uwanjani na acheni tuliocheza mpira wa Viwango vyetu na tunaoufuatilia 24/7 tutoe nyongo / hasira zetu. Ukweli utabaki pale pale kuwa Kocha Amunike alitepeta kama siyo kutokota katika Upangaji wa Timu jana na sasa ameanza Kutufanya wengine tuanze Kuhisi kuwa huenda ' alihongwa ' na ama Lesotho wenyewe au hata Cape Verde ili apange Kikosi cha ' Kipopoma ' ili tusifanye vizuri jana.
Acheni kutupandisha hasira zaidi kwa sababu zenu za Kipuuzi / Kipomboyo tafadhalini.