bene michael
Senior Member
- Mar 1, 2017
- 130
- 98
Na sijui kwanini ilimkosakosa na ndiyo maana leo hii anatusumbua hivi wana Simba SC.
Kwa mtazamo wangu usio wa kitaalamu sana,
1. Kama sheria hiyo ikipita, thamani ya simba iwe re-valued mpaka bilioni 120. Mo awe na wastani wa 11,1% ambayo ni bilioni 20 halafu wawekezaji wengine wa bilioni 40 watafutwe. Wanachama wawe na bilioni 61.2.
Kama hali itakubalika, zoezi la kuwatafuta hao wa kununua hizo bil. 40 liwe endelevu kidogo, kwa mfumo ambao utalazimisha kuwa marekebisho ya constitution ya bodi ya wakurugenzi yafanyike endapo muwekezaji anaweka mpaka asilimia kama 75 ya hisa anazonunua Cash, na mnunuzi wa mwisho atatakiwa kulipa asilimia 100 ili aingie kwenye bodi.
Kwanza bila hata mabadiliko ya sheria, thamani ya simba tayari imeshapanda hata sasa.
2. Kwa kuwa kuna maadui wa Simba, wanataka kuivuruga kabla mfumo wa kampuni haujakaa vizuri, nashauri watendaji chini ya mkurugenzi mtendaji, wawe na Mpango Mkakati (Strategic Plan) na Mpango wa Biashara (Business Plan). Simba ni moja ya makampuni ya Mo Dewji kwa sasa. Simba wanatakiwa kuwa na miradi ya kuingiza pesa kiujumla, pamoja na mambo ambayo Mo ameyaleta ambayo yana uwezo wa kuingiza pesa Simba.
3. Umuhimu wa Mo ni kuwa ameleta mtaji, maarifa na uzoefu wa kibiashara; wana Simba wameleta Jina; soko na pia maarifa. Ni vizuri kuwa sifa za pande mbili hizi zitumike kwa ajili ya masilahi mapana ya baadaye. Hatuna mashaka kuhusu uwezo wa kibiashara wa Mo Dewji na pia uwezo wa kimaarifa wa wanasimba kwa umoja wao.
4. Ni muhimu basi, bodi ipiganie shughuli za wazi za kuongeza kipato Simba: Estates( majengo yake) estate mpya ya bunju (mapato ya viwanja na hosteli) naamini timu ngeni zinaweza kuwa zinaweka kambi pale, mauzo ya wachezaji, na mapato mengine yatokanayo na performance: mapato yatokanayo na mataji n.k.
5. Wanaoisumbua Simba ni kwa kuwa wanaidharau kuwa inamtegemea mtu mmoja tu na akijitoa wamekwisha. Hakuna dawa zaidi ya kuongeza ukwasi kwa kutumia mfumo uliuopo, Mo Dewji akiwepo au (Mungu apishe mbali) asipokuwepo.