Waziri Mwigulu anatufanya Watanzania wote wajinga, atawezaje kutujaza wananchi shilingi trillion 5 mifukoni mwetu?

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,843
Reaction score
31,057
Hii siyo hadithi ambayo nimejitungia, bali nimemnukuu Waziri Mwigulu Nchemba, wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa benki mpya biashara Tanzania (TCB) siku 2 zilizopita, eti serikali yake ina mpango wa kutujaza wananchi shilingi trillion. 5 mifukoni mwetu, katika mzunguko wa pesa katika bajeti ya mwaka huu, kwa hiyo akatuhakikishia wananchi kuwa baada ya muda mfupi, hatutayasikia tena maumivu ya makato makubwa Sana, aliyoyaanzisha ya makato ya miamala ya simu.

Nilipomsikia waziri huyo akiyatamka hayo, nimeshangazwa sana na nikaona dhahiri kuwa waziri huyo ameanza kutapatapa kutokana na kilio kikubwa Sana cha wananchi kutokana na makato hayo ya wizi wa mchana kweupe wanayotufanyia wananchi wanyonge.

Nikajiuliza tena, kama serikali ya nchi yetu ingekuwa na ukwasi mkubwa kiasi hicho, je kulikuwa na sababu zipi za kuamua kuwakwamua watanzania tozo kubwa kiasi hicho?

Kwa kweli naona hivi sasa Waziri Mwigulu, ameanza kuweweseka kutokana na wananchi wengi kuamua kuzisusia huduma hizo za miamala ya simu na kuanza kutafuta mbadala wa miamala hiyo ya makampuni ya simu, hatua ambayo itawaacha mamilioni ya vijana, walioamua kujiajiri wakiwa hawana kazi za kufanya, baada ya kuvifunga vibanda vyao vya miamala ya simu.

Watanzania sasa hivi ndiyo wanaanza kushtuka baada ya Bunge lao kuwa la chama kimoja cha CCM, kuwa kila kinacholetwa na serikali, hata kama ni cha ukandamizaji na dhuluma kiasi gani, ni lazima kitapita!

Ndipo hapo watanzania tunaona umuhimu wa kuwa na Katiba mpya ya nchi, ambayo haitawafanya wanaccm, ambayo itatupa Time huru ya uchaguzi na siyo hii ya sasa, ambayo Mwenyekiti wa CCM wa Taifa, ndiyo mwenye mamlaka ya kuteua makamishna wote wa Tume ya uchaguzi na hivyo kujiona wao CCM, kuwa ndiyo wenye hati miliki ya kuitawala nchi yetu milele na milele!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…