Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 itasomwa leo tarehe 13 Juni, 2024 Bungeni Jijini Dodoma.
======
Mwigulu amenza kusoma bajeti na anaanza kwa kuzitaja shabaha za uchumi
Waziri Mwigulu amemshuru Rais Samia kwa uongozi shupavu uliodhihirishwa na majira nchi iliyopitia ikiwemo kupwemo nchi ikiwa imekumbwa na huzuni ya kuondokewa na aliyekuwa Rais na nchi inasonga mbele.
Mwigulu amesema alipokea nchi ikiwa na janga la uviko19 na baadae vita ya Ukraine lakini aliendelea na miradi iliyokuwepo na kuleta mingine mipya.
MAFANIKIO
MWIGULU NCHEMBA
Usimamizi wa Matumizi ya Fedha za Umma
Serikali imefanya uwekezaji mkubwa kwenye mifumo ya uendeshaji wa shughuli zake ili kudhibiti matumizi ya fedha za umma. Hata hivyo, mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amekuwa akitoa hoja zinazohusu matumizi ya fedha za umma.
Serikali itaendelea kuhakikisha Sheria hizo zinasimamiwa na kutekelezwa ipasavyo ikiwa ni pamoja na kujibu hoja zilizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na hoja za wakaguzi wa ndani.
Maslahi ya Watumishi na Wastaafu
Serikali imeendelea kuhakikisha kuwa malimbikizo ya kimshahara na yasiyo ya kimshahara ya watumishi wa umma yanalipwa kwa wakati. Katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Sita, jumla ya shilingi bilioni 98.63 zimelipwa kama malimbikizo mbalimbali ya watumishi wa umma.
Aidha, katika kipindi hicho, Serikali imelipa jumla ya shilingi bilioni 160.04 kwa ajili ya kugharamia upandishwaji wa vyeo kwa watumishi wa umma wapatao 126,814 katika kada mbalimbali.
Kikokotoo
Mwigulu Nchemba: Hata hivyo, kumekuwa na kilio kikubwa kutoka kwa wastaafu kuhusu kikokotoo. Mheshimiwa Spika, mabadiliko ya kikokotoo yalishusha kundi la wafanyakazi waliokuwa wakipokea mkupuo wa asilimia 50 mpaka asilimia 33, na kundi waliokuwa wakipokea asilimia 25 walipandishwa mpaka asilimia 33.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameelekeza kuongezwa malipo ya mkupuo kutoka asilimia 33 iliopo sasa hadi asilimia 40.
Hili ndio kundi kubwa la watumishi wakiwepo, Walimu, kada ya afya, Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto na makundi mengine yaliyopo Serikali kuu na Serikali za Mitaa.
Rais ameelekeza kuongezewa zaidi kundi lililokuwa likipokea asilimia 25 hapo awali na kupandishwa kwenda asilimia 33 sasa itakuwa asilimia 35 kuanzia mwaka wa fedha huu.
Serikali itaendelea kuangalia maslahi ya wastaafu kwa kuzingatia tathmini ya uhai na uendelevu wa mifuko.
Kuimarisha Upatikanaji wa Fedha za Kigeni
Mheshimiwa Spika, kama ilivyokuwa kwa nchi nyingi duniani, nchi yetu pia ilikabiliwa na changamoto ya upungufu wa fedha za kigeni mwaka 2023/24. Changamoto hii ilisababishwa na mambo mbalimbali ikiwemo: athari za UVIKO–19; vita vinavyoendelea nchini Ukraine na katika ukanda wa Gaza; mabadiliko ya tabianchi; na kubadilika kwa sera za fedha katika nchi zilizoendelea.
Changamoto hizo zilisababisha kupanda kwa riba za fedha kwenye nchi zilizoendelea na masoko ya kimataifa ili kukabiliana na mfumuko wa bei kwenye nchi hizo. Hali hiyo ilipunguza ukwasi na mzunguko wa fedha za kigeni katika uchumi wa dunia kwa ujumla.
Mheshimiwa Spika, pamoja na changamoto hii kuwa kubwa katika nchi nyingi duniani, Serikali ilifanikiwa kukabiliana nayo kwa kushirikiana na sekta binafsi na washirika wa maendeleo ili kuendelea kuwa na akiba ya kutosha ya fedha za kigeni.
Hadi Machi 2024, akiba ya fedha za kigeni ilikuwa dola za Marekani bilioni 5.3, kiasi ambacho kinakidhi uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje kwa miezi 4.4, ambacho kiko juu ya lengo la nchi la muda usiopungua miezi 4.0.
Mheshimiwa Spika, kuanzia tarehe 1 Julai, 2024,naelekeza wadau wote wa ndani, taasisi za umma, wafanyabiashara, asasi za kiraia, mashirika ya kimataifa na watu wote waliopo nchini Tanzania wenye tabia ya kuweka bei kwenye huduma au kuuza bidhaa kwa fedha za kigeni kuacha mara moja na kuhakikisha bei za bidhaa na hudumahizo zinatangazwa na kulipwa kwa Shilingi ya Tanzania.
Aidha, nazielekeza taasisi zote za Serikali zinazotoza ushuru, ada na tozo mbalimbali kwa fedha za kigeni kurekebisha kanuni zao ili tozo hizo zilipwe kwa shilingi. Hata mgeni akija na fedha za kigeni ni vyema akaibadilisha kuwa fedha ya kitanzania ili aweze kupata huduma. Tunafanya kila malipo kwa fedha za kigeni, halafu shilingi ikishuka thamani tunajiuliza tumekosea wapi.
Pia, SOMA
- Luhanga Mpina apewa siku 10 na Spika kuleta ushahidi wa Bashe kulidanganya Bunge
======
- Kuongeza kasi ya ukuaji wa pato la Taifa kufikia 5.4% kwa mwaka 2024
- Kuendelea kudhibiti kasi ya mfumuko wa bei wa wastani wa asilimia 3-5.
- Mapato ya ndani kufikia 15.8% ya pato la Taifa kwa mwaka 2024/25
- Mapato ya kodi kufikia 12.4% kwa mwaka 2024/25
- Kuwa na nakisi ya bajeti inayojumuisha misaada isiyozidi 3% ya pato la Taifa
- Kuwa na akiba ya fedha za kigeni kwa kiwango cha kukidhi mahitaji kwa kipindi kisichopungua miezi minne.
- Kuchochea uchumi shindani na shirikishi.
- Kuimarisha uwezo wa uzalishaji viwandani na utoaji huduma
- Kukuza biashara na uwekezaji
- Kuchochea maendeleo ya watu na kuendeleza rasilimali watu
- Kukamilisha miradi ya kielelezo na ya kimkakati
- Kuimarisha sekta za uzalishaji
- Kuimarisha rasilimali watu hususan sekta za jamii
- Kuongeza matumizi ya Tehama
- Kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji wa sekta binafsi
- Kugharamia mishahara ya watumishi wa umma
- Deni la Serikali
- Uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa mwaka 2024 na maandalizi ya uchaguzi mkuu mwaka 2025
- Maandalizi ya dira ya maendeleo 2050
Waziri Mwigulu amemshuru Rais Samia kwa uongozi shupavu uliodhihirishwa na majira nchi iliyopitia ikiwemo kupwemo nchi ikiwa imekumbwa na huzuni ya kuondokewa na aliyekuwa Rais na nchi inasonga mbele.
Mwigulu amesema alipokea nchi ikiwa na janga la uviko19 na baadae vita ya Ukraine lakini aliendelea na miradi iliyokuwepo na kuleta mingine mipya.
MAFANIKIO
- Uchukuzi, alipokea mradi wa reli ukiwa 57% na 83.5% kwa loti ya pili na kwanza lakini hadi sasa loti ya Dar hadi Dodoma imeshakamili, imeshajaribiwa na nauli imeshatangazwa takribani 31,000.
- Miradi mipya, lot 3 mpaka 6 ambazo ni kuanzia Makutupora mpaka Msongati
- Bandari, kuongeza kina kufikia mita 15.5 na upana wa mita 200 katika lango la kuingia na kugeuzi meli. Pia Serikali itaendelea na ujenzi wa bandari kavu ya Kwala na ujenzi wake umeshafikia 96%.
- Anga, ujenzi wa viwanja vya ndege ikiwemo Msalato
- Usafiri na usafirishaji, barabara zinajengwa kupitia Tanroads na Tarura. Bajeti ya Tarura imeongezeka kutoka bilioni 710 kufikia 841 mwaka wa fedha 2025.
- Daraja la Kingongo-Busisi lilifikia zaidi ya 88%
- Nishati, JNHPP alipokea ikiwa takribani 37% na sasa upo katika hatua za mwisho na kujaribiwa na sasa zinapatikana megawatts 235 na kuongezwa kwenye upatikanaji wa umeme na ndio maana nchi imetoka kwenye katikakatika ya umeme na mgao wa umeme ambao ulishaanza kulikumba Taifa letu.
MWIGULU NCHEMBA
Usimamizi wa Matumizi ya Fedha za Umma
Serikali imefanya uwekezaji mkubwa kwenye mifumo ya uendeshaji wa shughuli zake ili kudhibiti matumizi ya fedha za umma. Hata hivyo, mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amekuwa akitoa hoja zinazohusu matumizi ya fedha za umma.
Serikali itaendelea kuhakikisha Sheria hizo zinasimamiwa na kutekelezwa ipasavyo ikiwa ni pamoja na kujibu hoja zilizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na hoja za wakaguzi wa ndani.
Maslahi ya Watumishi na Wastaafu
Serikali imeendelea kuhakikisha kuwa malimbikizo ya kimshahara na yasiyo ya kimshahara ya watumishi wa umma yanalipwa kwa wakati. Katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Sita, jumla ya shilingi bilioni 98.63 zimelipwa kama malimbikizo mbalimbali ya watumishi wa umma.
Aidha, katika kipindi hicho, Serikali imelipa jumla ya shilingi bilioni 160.04 kwa ajili ya kugharamia upandishwaji wa vyeo kwa watumishi wa umma wapatao 126,814 katika kada mbalimbali.
Kikokotoo
Mwigulu Nchemba: Hata hivyo, kumekuwa na kilio kikubwa kutoka kwa wastaafu kuhusu kikokotoo. Mheshimiwa Spika, mabadiliko ya kikokotoo yalishusha kundi la wafanyakazi waliokuwa wakipokea mkupuo wa asilimia 50 mpaka asilimia 33, na kundi waliokuwa wakipokea asilimia 25 walipandishwa mpaka asilimia 33.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameelekeza kuongezwa malipo ya mkupuo kutoka asilimia 33 iliopo sasa hadi asilimia 40.
Hili ndio kundi kubwa la watumishi wakiwepo, Walimu, kada ya afya, Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto na makundi mengine yaliyopo Serikali kuu na Serikali za Mitaa.
Rais ameelekeza kuongezewa zaidi kundi lililokuwa likipokea asilimia 25 hapo awali na kupandishwa kwenda asilimia 33 sasa itakuwa asilimia 35 kuanzia mwaka wa fedha huu.
Serikali itaendelea kuangalia maslahi ya wastaafu kwa kuzingatia tathmini ya uhai na uendelevu wa mifuko.
Kuimarisha Upatikanaji wa Fedha za Kigeni
Mheshimiwa Spika, kama ilivyokuwa kwa nchi nyingi duniani, nchi yetu pia ilikabiliwa na changamoto ya upungufu wa fedha za kigeni mwaka 2023/24. Changamoto hii ilisababishwa na mambo mbalimbali ikiwemo: athari za UVIKO–19; vita vinavyoendelea nchini Ukraine na katika ukanda wa Gaza; mabadiliko ya tabianchi; na kubadilika kwa sera za fedha katika nchi zilizoendelea.
Changamoto hizo zilisababisha kupanda kwa riba za fedha kwenye nchi zilizoendelea na masoko ya kimataifa ili kukabiliana na mfumuko wa bei kwenye nchi hizo. Hali hiyo ilipunguza ukwasi na mzunguko wa fedha za kigeni katika uchumi wa dunia kwa ujumla.
Mheshimiwa Spika, pamoja na changamoto hii kuwa kubwa katika nchi nyingi duniani, Serikali ilifanikiwa kukabiliana nayo kwa kushirikiana na sekta binafsi na washirika wa maendeleo ili kuendelea kuwa na akiba ya kutosha ya fedha za kigeni.
Hadi Machi 2024, akiba ya fedha za kigeni ilikuwa dola za Marekani bilioni 5.3, kiasi ambacho kinakidhi uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje kwa miezi 4.4, ambacho kiko juu ya lengo la nchi la muda usiopungua miezi 4.0.
Mheshimiwa Spika, kuanzia tarehe 1 Julai, 2024,naelekeza wadau wote wa ndani, taasisi za umma, wafanyabiashara, asasi za kiraia, mashirika ya kimataifa na watu wote waliopo nchini Tanzania wenye tabia ya kuweka bei kwenye huduma au kuuza bidhaa kwa fedha za kigeni kuacha mara moja na kuhakikisha bei za bidhaa na hudumahizo zinatangazwa na kulipwa kwa Shilingi ya Tanzania.
Aidha, nazielekeza taasisi zote za Serikali zinazotoza ushuru, ada na tozo mbalimbali kwa fedha za kigeni kurekebisha kanuni zao ili tozo hizo zilipwe kwa shilingi. Hata mgeni akija na fedha za kigeni ni vyema akaibadilisha kuwa fedha ya kitanzania ili aweze kupata huduma. Tunafanya kila malipo kwa fedha za kigeni, halafu shilingi ikishuka thamani tunajiuliza tumekosea wapi.
Pia, SOMA
- Mwigulu: Kutoza ndani ya nchi kwa dola ni kosa, watakiwa kuacha kuanzia Julai mosi
- Mwigulu Nchemba: Tsh Trilioni 5 za deni la taifa zimeongezeka kutokana na kushuka kwa thamani ya shilingi
- Mwigulu ataka makosa ya barabarani yachukuliwe serious zaidi kuliko ilivyo sasa
- Hali ya uchumi ya Taifa 2023 na mpango wa maendeleo wa Taifa 2024-25
- Tanzania ya uchumi wa kidijitali yanukia kuelekea 'Cashless economy'
- Hatimaye Kikokotoo kimeanza kulegezwa
- Watumiaji wa gesi asilia kwenye magari wamefikiwa, wawekewa tozo ya 382 kwa kila kilo
- Mwigulu Nchemba: Serikali imebaini Mawakala wakusanya kodi ambao sio waaminifu katika kutimiza majukumu yao
- Mwigulu Nchemba: Tsh. Trilioni 5 za Deni la Taifa zimeongezeka kutokana na kushuka kwa Thamani ya Shilingi
- Waziri Mwigulu: Wanasiasa waliofilisika wanatafuta uhalali wa kisiasa kwa ubaguzi ni hatari na wa hovyo
- Waziri Mwigulu: Kutoza ndani ya nchi kwa dola ni kosa, watakiwa kuacha kuanzia Julai mosi
- Waziri wa Fedha asema Tsh. Bilioni 136.2 zimetumika urejeshaji wa Miundombinu barabara na madaraja
- Waziri Mwigulu: Nauli ya Dar kwenda Dodoma kwa treni ya Standard Gauge ni Takriban 30,000