Waziri Mwigulu: Baadhi ya waliopotea wanahusika na uhalifu

funaku

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
39,468
Reaction score
31,952
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba akijibu hoja mbalimbali za wabunge, ameeleza kuwa baadhi ya watu waliopotea nchini wanahusika na vitendo vya uhalifu

Dkt. Nchemba amefafanua kuwa wapo watu waliokimbia familia zao kutokana na kujihusisha na biashara ya Dawa za Kulevya, ujambazi na mengineyo

Chanzo: Taarifa ya Habari TBC mchana wa leo
 
Ningependa wale wanaosema wamepotelewa na ndugu au jamaa wawe kwenye orodha rasmi, maana yaonekana wengi wetu tumekuwa wazushi kwa kung'ang'ania watu kuuawa au kupotea, cha kushangaza wale wanaolalamika hatuwaoni kwenye mitandao kusema ndugu yangu, jamaa yangu n.k. haonekani, polisi wameomba wote waliopoteza jamaa zao kuepeleka taarifa, cha kushangaza ni wachache mno, na sababu zao zinajulikana!
Ni uzuzu uliokomaa na kupindukia kukoleza ya kupotea na kuuawa kwa watu kama wewe binafsi hujapoteza mtu..
Matokeo ya haya mmeona Bw. Nondo alivyoponzeka..
 

Kama Mayalla kuitwa tu na kuhojiwa kanyamaza kimya hasikilikani tena na ni mtu ambaye mlokua mnamtegemea hapa jf, je watu wanyonge unategemea watapata wapi nguvu ya kuonekana kwenye vyombo vya habari wakalalamika. Au unataka na hao wakamalizwe

Kuna chombo gani cha habari kiko huru kwenda kutafuta habari zao?
 
Ben Saa 8 na AZORY
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…