Waziri Mwigulu: Kutoza ndani ya nchi kwa dola ni kosa, watakiwa kuacha kuanzia Julai mosi

Tamko hili halijawahi kubadili utaratibu wa ubadilishaji wa fedha.
Soko huria linaamuliwa kwa nguvu ya "uhitaji na kilichopo sokoni"(Demand and Supply).
sera,kubadilika mara kwa mara na kukosa misimamo katika bei za bidhaa inaleta hofu na hivyo kusababisha bei kupanda hovyo na hivyo kushusha thamani ya shiĺingi.

Kama Serikali inataka kudhibiti mfumko wa bei,hakikisheni EWURA,na LATRA wanaacha kutoa matamko ya kupandisha nauli na bei za mafuta baada ya bajeti kupitidhwa.

Mfano EWURA kila mwezi anapandisha bei,unakuta leo anaita vyombo vya habari na kutangaza bei yamafuta kwa mwezi ujao(mbona bidhaa zingine hazipangiwi bei mwezi mmoja kabla?,Hii Marehemu Rais wa Awamu ile alikemea na hatukuona bei zinapanda kiholela).

Ushauri,Serikali idhibiti kupanda kwa bei mbalimbali,na kudhibiti matumizi ya Serikali ili tuimarishe shilingi, na kusaidia bei kushuka.
 
Mikataba ya Dola pia iondolewe ndipo tutapata ahueni ya shilingi
 
Mwigulu yupo sahihi kama akiweza...Botswana au SA hakuna upuuzi wa usd pale kila kitu ni Rand au Pula hata hapo Namibia hizi mambo za usd dola sijui wajinga walizotoa wapi...
Botswana ndio Nchi Afrika unatoa dola mia unapewa pula Tisini...
 

Nosense!!

Kinachotakiwa ni kuipa thamani shilingi ili watu wenyewe wakimbilie kuipata shilingi.

Hata Russia, vita ilipozuka tu, kila mmoja alihangaika kupata sarafu ya nchi nyingine, kama dola, pound na Euro, kwa sababu ya hofu. Rubo ikadondoka kwa 40% wiki ya kwanza.

Mikakati ya kusimamia uchumi ilo wa usiyumbe kutokana na vita, iliwafanya wananchi watulie, wasihamgaike kutafuta pesa za kigeni, na rubo ikaimarika.

Sasa huyu mjinga anadhani unaweza kuiimarisha shilingi kwa kauli badala ya mbinu za kiuchumì.
 
Kauli kama hizi azikuanza leo, ngoja tuone wao wenyewe rushwa wanachukua kwa dola na siyo pesa za madafu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…