Waziri Mwigulu: Kutoza ndani ya nchi kwa dola ni kosa, watakiwa kuacha kuanzia Julai mosi

Waziri Mwigulu: Kutoza ndani ya nchi kwa dola ni kosa, watakiwa kuacha kuanzia Julai mosi

Tamko hili halijawahi kubadili utaratibu wa ubadilishaji wa fedha.
Soko huria linaamuliwa kwa nguvu ya "uhitaji na kilichopo sokoni"(Demand and Supply).
sera,kubadilika mara kwa mara na kukosa misimamo katika bei za bidhaa inaleta hofu na hivyo kusababisha bei kupanda hovyo na hivyo kushusha thamani ya shiĺingi.

Kama Serikali inataka kudhibiti mfumko wa bei,hakikisheni EWURA,na LATRA wanaacha kutoa matamko ya kupandisha nauli na bei za mafuta baada ya bajeti kupitidhwa.

Mfano EWURA kila mwezi anapandisha bei,unakuta leo anaita vyombo vya habari na kutangaza bei yamafuta kwa mwezi ujao(mbona bidhaa zingine hazipangiwi bei mwezi mmoja kabla?,Hii Marehemu Rais wa Awamu ile alikemea na hatukuona bei zinapanda kiholela).

Ushauri,Serikali idhibiti kupanda kwa bei mbalimbali,na kudhibiti matumizi ya Serikali ili tuimarishe shilingi, na kusaidia bei kushuka.
 
Mwigulu ameongelea watanzania kulikuza tatizo la upungufu wa dola kudai au kufanya malipo ya bidhaa na huduma zinazotolewa ndani ya nchi kwa kutumia fedha ya kigeni. Mwigulu amesema kulipa kwa fedha za kigeni nchini kunaifanya shilingi ikose thamani na dola kuwa na thamani ndani ya nchi.

Mwigulu amesema kuuza bidhaa au huduma kwa kutumia fedha za kigeni ni kosa kwa mujibu wa kifungu cha 26 cha sheria ya benki kuu ya mwaka 2006 ambacho kinabainisha shilingi ya Tanzania ndio fedha pekee ya malipo ndani ya nchi.

Mwigulu amehimiza wananchi na wadau kuacha kulipa au kununua vitu kwa fedha za kigeni kwani ni haki kisheria kwa kutumia sarafu ya shilingi.

Mwigulu ameielekeza benki kuu na vyombo vingine kuratibu jambo hilo kwa ufanisi.

Hatua nzuri lakini nimkumbushe Mwigulu kuna baadhi ya taasisi za Serikali zinadai malipo ya fedha za kigeni hasa kwa wageni na ni hitaji la lazima.
Mikataba ya Dola pia iondolewe ndipo tutapata ahueni ya shilingi
 
Mwigulu yupo sahihi kama akiweza...Botswana au SA hakuna upuuzi wa usd pale kila kitu ni Rand au Pula hata hapo Namibia hizi mambo za usd dola sijui wajinga walizotoa wapi...
Botswana ndio Nchi Afrika unatoa dola mia unapewa pula Tisini...
 
Mwigulu Nchemba akisoma bajeti ya serikali bungeni amesema suala la taasisi binfasi na za umma kutaka malipo ya huduma kwa fedha za kigeni zinaleta shida kwa watanzania kwa kuwa wanatumia Tsh na sio dola.

Amesema suala hili linafanya watanzania kuhangaika kuipata dola, wakati inabidi hata wageni wakija nchini wahangaike kuipata shilingi na sio dola. Kutokana na jambo hilo amesema kuwa kuanzia Julai 1, 2024 malipo yote kwa taasisi za umma na binafsi watatakiwa kupokea malipo kwa shilingi tu.

Aidha amesema kama mtu atakuja na fedha za kigeni, atatakiwa kwanza kuzibadilisha na kupata shilingi ya Tanzania ili kufanya malipo

===

Pia soma:
- News Alert: - Waziri Mwigulu awasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025

Nosense!!

Kinachotakiwa ni kuipa thamani shilingi ili watu wenyewe wakimbilie kuipata shilingi.

Hata Russia, vita ilipozuka tu, kila mmoja alihangaika kupata sarafu ya nchi nyingine, kama dola, pound na Euro, kwa sababu ya hofu. Rubo ikadondoka kwa 40% wiki ya kwanza.

Mikakati ya kusimamia uchumi ilo wa usiyumbe kutokana na vita, iliwafanya wananchi watulie, wasihamgaike kutafuta pesa za kigeni, na rubo ikaimarika.

Sasa huyu mjinga anadhani unaweza kuiimarisha shilingi kwa kauli badala ya mbinu za kiuchumì.
 
Kauli kama hizi azikuanza leo, ngoja tuone wao wenyewe rushwa wanachukua kwa dola na siyo pesa za madafu...
 
Back
Top Bottom