Waziri Mwigulu, kwanini Serikali ikope Trilion 6 kufadhili budget ilhali DP World wapo?

Unajua maana ya break even point?
Break Even Point- Is the point at which total cost is equal to total cost, meaning, there is no profit and no loss!!

Kwa Tafsiri ya kiswahili,

Ni hatua ambayo biashara Iko hatua ambayo mapato na matumizi Yako sawa, hakuna HASARA, pia hakuna faida.

Swali ni Moja tu: DP World wamewekeza shilingi ngapi mtaji wao ambao tunaweza uita gharama ya uwekezaji, lakini mapato Kila siku yanaingia?

Bandari walijenga wao?
 
Kawekeza bei gani si wanaojua ni Serikali, kama mkataba haujapelekwa bungeni kama sheria ya TEIT na sheria ya natural resources and Permanent sovereign act then ni udhaifu wa bunge sio serikali.

issue ni kwamba wao wame lease bandari kwa minajili ya kwamba Dp world wanatoa gharama za uendeshaji na profit margin yao the rest inaenda hazina. Ni kawaida ya concession agreements duniani kote sawa tu na NAS au Swiss port kupakua mizigo Airport mbona huwa hatusemi tumeuza Airport kwa waarabu na wazungu?

Nadhani mambo ya kitaaluma waachiwe wana taaluma sio laymen.
 
Mimi na wewe ndio Serikali,

Ikiwa Hadi sasa sijui DP World wamewekeza Bei Gani, unawezaje uita huo ni mkataba?

Na ikiwa hawajauza, kwamba wamekodisha, kwanini wasichukue advance ya Trillion 6 kufadhili budget?

Hawajawekeza hata mia katika kujenga bandari, iweje tuhangaike?

Mwisho niseme, Layman/ laywoman ni Babu na bibi Yako!!
 
Concession agreements huwa zikoje? Jibu kwanza hilo ndio nitajua uelewa wako juu ya mikataba ya uwekezaji.
 
KIKOKOTOO NI WIZI, KATAA KIKOKOTOO KINAUA WASTAFU
 
Budget inafadhiliwa?
 
Dp world yaweza ikawa Haina tofauti na kADC ya KIA
Tofautu ninkubwa sana, jdac hata mwenyewe alikuwa hajulikani ni nani, DP World ni jampuni ya Kimataifa.

Usilinganishe tembo na funza.
 
Kwani bandari ni mali ya Dp world au watanzania?
Bandari ni ya Watanzania mwendeshaji baadhi ya eneo la bandari ni DP World.


.Watanzania tulishindwa kuendesha bandari kwa ufanisi kama tunavyoshindwa kwenye mwendo kasi na mashirika mengine yote ya umma.
 
Unanikumbusha tatizo la kuhoji ambalo linaanzia ngazi ya familia, swali hivi Burundi tumepakana nayo?
 
Unanikumbusha tatizo la kuhoji ambalo linaanzia ngazi ya familia, swali hivi Burundi tumepakana nayo?
Ndio Mwigulu, Burundi tumepakana nayo!!

Je Burundi inahusiana na MADA hapo juu?
 
Nadhani ni mapema mno kuanza kuhoji hivyo wakati DP World imeanza kazi mwezi uliopita!
 
Nadhani ni mapema mno kuanza kuhoji hivyo wakati DP World imeanza kazi mwezi uliopita!
Kwamba Serikali tangu DP World akabidhiwe, haijapata hata mia mbovu?

Shughuli na mapato hayakuwahi kusimama!!

Hiyo mikataba ingewekwa wazi, maswali mengi yangeshajibiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…