Waziri Mwigulu: Makato ya Miamala ya Simu tunatunisha mfuko, ni 'Solidarity Fund'

Waziri Mwigulu: Makato ya Miamala ya Simu tunatunisha mfuko, ni 'Solidarity Fund'

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
"Mtu anayetuma 1000 hadi 2000 anakatwa Tsh.10, anayetuma 20,000 hadi 30,000 anakatwa 960, Mil. 1 hadi Mil. 3 ni 9000 na Mil 3 na kuendelea ni 10,000, kwa anaetuma 100,000 hadi 200,000 anakatwa 2500, kama unaweza kutuma 10,000 kwanini usichangie shughuli za maendeleo?”

"Mimi naunga mkono dira ya Rais ya kutaka maji yapatikane kila kijiji, sasa tunafanyaje? tukasema tuchangishane, hivi unaona tunaweza kupoteza maisha ya Mtoto sababu ya maji, kisa unalia unakatwa Tsh.5?, mbona milio ya simu tunaweka na unakatwa Tsh. 100?"

"Kuna Shule zinakusanya watoto mpaka 1500 au 1000 na Shule haina maji wanaambiwa waende Shule na kidumu cha maji, sasa tunafanyaje ili maji yapatikane? ndio maana kuna uwepo wa kukatwa Tsh. tano kila unapotuma hela kwa ajili ya huu mfuko wa mshikamano"

"Watu wanalalamika kuhusu hela za miamala, hii ni solidarity fund, tuna mambo ambayo tunakubaliana hayapaswi kuendelea mfano ubovu wa Barabara vijijini, kama Taifa tuongeze Tsh.100 katika mafuta ili kila fedha itakayoongezeka iende kuleta maendeleo"

"Kwenye chungu, ni lazima bajeti, fedha zitatoka wapi ni lazima tutoe kodi, mwaka huu tumeleta kodi ya miamala, ni vizuri sana mjue hili la kwenye miamala sio tu kodi, hili tunatunisha mfuko, ni solidarity fund, huu ni mfuko wa mshikamano wa Watanzania"

"Akaunti zilifungwa kipindi kile kwasababu ya masuala ya kikodi na Wafanyabiashara wanarudishiwa fedha zao kwasababu akaunti imelipa kodi au hesabu zake zilipigwa vibaya kwahiyo kuna fedha ambayo haikuwa kodi inarudishwa"

"Kenya, Uganda, Malawi, Rwanda, Msumbiji mafuta yako bei juu kuliko sisi, ulishaona hizo Nchi waje kununua mafuta Tanzania?, nitoe rai Watanzania wawe Wazalendo kwasababu kwenye Nchi zote zinazotuzunguka Tanzania ndio Nchi inayouza mafuta bei ya chini"

Chanzo: CLOUDS 360
 
Wazo zuri la kuchangia ila matumizi yenu nyine kina mwigulu ni anasa sana, wananchi wapo wiling kuchanga ila nyie hamjibani ,mnazidi kununua mavx ya milioni 400 kila moja, ma perdiem yasiyo na kichwa wala miguu wakati tuna mkongo wa taifa, tuna zoom, yaani unafunga safari ya zaidi ya km 600 na msafara wa magari 20 kwenda kukata utepe? Kama kuchangia mbona nyinyi viongozi hamchangii yaani wanachangia walalahoi tu?
 
Waziri anasema ni solidarity, lakini haihusu posho zao.
Yaonekana ni kazi ngumu sana kumpata mtu anayestahili kuwa waziri. Hayo ndo maelezo ya mtu anayeitwa waziri? Kama ni mapungufu ya akili, hii inazidi kipimo. Ni aibu kwa waziri kuwaambia wananchi wake kwamba sasa anakusanya solidarity bila wao kupenda.

Hadithi za watoto, maji, barabara, na upuuzi mwingine zitakwenda kwa solidarity za aina hii kweli? Mara reli, REA, ..... Pumbaf!
 
CCM wanavyofanya ni sawa waliiba kura wakafanyikiwa kujipachika madaraka, siwezi kushangaa chochote watakachofanya ni sawa acha wafanye acha watafute pesa za kuvuruga na kupanga matokeo ya uchaguzu ujao,sisi yetu macho
 
Wazo ni zuri sana iwapo tu wale majambazi ndani ya chama na serikali hawataamua kujinemeesha kwa jasho la mwananchi anaenda kukatwa hiyo pesa. Chama changu na serikali yangu ina majambazi waliongia kwa gia ya kuwaongoza wananchi huku wakipora jasho la wanyonge na hata rasili mali za nchi hii.

Ifike mahali kila mkoa au wilaya ikusanye na kuamua matumizi ya mapato yake ya mdani na serikali ibaki kuwa msimamizi na mhakikishaji kuwa mapato yanatumika vyema, lakini pia kutoa rudhuku kwa wilaya zisizo na uwezo kwa kupitia kodi kama hizi zinazogusa wananchi wote nchini.
 
"Mtu anayetuma 1000 hadi 2000 anakatwa Tsh.10, anayetuma 20,000 hadi 30,000 anakatwa 960, Mil. 1 hadi Mil. 3 ni 9000 na Mil 3 na kuendelea ni 10,000, kwa anaetuma 100,000 hadi 200,000 anakatwa 2500, kama unaweza kutuma 10,000 kwanini usichangie shughuli za maendeleo?”...
Pumbavu zake! Solidarity hailazimishwi bali ni hiari!
 
Badala ya kuvifuta vyeo vya kipuuzi kama vya wakuu wa mikoa na wilaya, kuondoa wabunge wa viti maalum na wale wa kuteuliwa! Kuondoa vyeo vya Ma Ras na Ma das, kupeleka mswada wa kupunguza posho nono wanazolipwa bungeni!

Yeye anakimbilia kwenye TOZO!! Kuna mijitu ni Mibinafsi, ila miana siasa aina ya Mwigulu Nchemba, imepitiliza aisee!!
 
Back
Top Bottom