Waziri Mwigulu: Makato ya Miamala ya Simu tunatunisha mfuko, ni 'Solidarity Fund'

Waziri Mwigulu: Makato ya Miamala ya Simu tunatunisha mfuko, ni 'Solidarity Fund'

Inasikitisha sana kuwa mtu kama huyu ndio waziri wa fedha na hayo ndio maelezo yake anayotoa kuhalalisha ujinga wao.

Yani kigezo cha kumtoza mtu zaidi ni kwa vile ana uwezo wa kutuma elfu 10? Alishajiuliza hiyo elfu 10 anayoona yeye ndogo huyo mtu kaipataje ama ina thamani gani kwake?

Shule hazina maji, hilo linakuaje suala la kubebeshwa mwananchi baada ya miaka zaidi ya 50 ya kuwa madarakani serikali hiyo hiyo moja?

Sio kweli kuwa Tanzania mafuta ni bei rahisi zaidi, aende Zambia tu hapo akaone bei ya mafuta na ajabu zaidi wanapitishia mafuta hayo hapa kwetu.

Hii nchi tumekalia udaku wa kina Mwijaku instagram wakati mambo ya msingi yanachukuliwa kiwepesi wepesi tu.
 
Kuna ulazima wa kupunguza idadi ya wabunge kwa asilimia 50.
Fikiria huyu ni waziri wa fedha ndio ubunifu wake umeishia kuwakamua wanyonge mara dufu.
 
Serikali ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuendelea kuiunganisha nchi kwa kutengeneza miundombinu mipya ya barabara katika maeneo yasiyofikika ambayo kwa asilimia kubwa yapo vijijini.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amesema ili kuhakikisha kwamba lengo la Mhe. Rais la kuinua uchumi linafanikwa kama alivyoahidi ameanza kwa kutengeneza miundombinu ya barabara za Vijijini kupitia ongezeko la Shilingi 100 kitakachopatikana kwenye mafuta ambapo Serikali itakusanya zaidi ya Shilingi Bilioni 322.

Waziri Nchemba amesema barabara za Vijijini zikishakamilika itapunguza vifo vya Mama Wajawazito ambao kwenye maeneo mengi wanajifungulia njiani sababu ya barabara hazipitiki, lakini pia itasaidia maeneo yasiyokua na maendeleo kupata maendeleo kwa kasi.

Hakika Mama hakukosea aliposema nia yake ni kuisimamisha nchi kiuchumi, na kazi hiyo anaifanya kwa kasi kubwa sana, muhimu Watanzania tuendelee kumuombea na kulipa kodi kihalali.
 
Waziri zero kichwani kuwahi kutokea tokea nchi imepata uhuru mwaka 1961 huko.

Yeye ni Waziri Wa Fedha, ameamua kutunyonga watanzania kwenye mafuta, fresh tu, badala ya 100/= aongeze hata 5,000/= katika kila lita moja. Ila atabakia kuwa Waziri asiekua na akili hata ya kuchambia, maswala ya ujenzi wa barabara hana mamlaka nayo, hayo maswala ni ya kuongelewa na Waziri/Naibu Wa Maswala Ya Ujenzi Na Miundombinu au TanRoads.

Huyu Mwigulu asipoelekezwa mipaka na majukumu ya Wizara Yake, basi kuna siku atakuja hata kumuingilia CDF Mabeyo kwenye mamlaka yake ya kijeshi.

Hii nchi hata Pierre Likwid akipewa uwaziri, mbona ataongoza wizara vizuri kuliko hawa wanaojiita wasomi.
 
Kila mwaka huwa wanapandisha kodi kwenye bidhaa zile zile zenye umuhimu kwa wananchi, halafu wanajisifu kwa ubunifu wao.

Mwigulu anataka kusema amekosa kabisa chanzo kingine cha mapato zaidi ya kumnyonya mwananchi wa kawaida kwenye bidhaa adimu wanayoitumia kila siku?

Kule kwenye machimbo ya madini mliyowapa wazungu kwa kuchukua 10% pangefaa zaidi kuwaongezea kodi wale wafanyabiashara kutokana na faida wanayopata, kuliko kuyafanya mafuta yaonekane anasa.

Kwa hali hii mnaondoa vipi umasikini kwa mwananchi wa kawaida hasa kule vijijini kama bado mnamuongezea mzigo matumizi kwenye mahitaji yake muhimu? hata tukiwatumia pesa za matumizi kwa njia ya simu nako mmepandisha kodi!.
 
Serikali ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuendelea kuiunganisha nchi kwa kutengeneza miundombinu mipya ya barabara katika maeneo yasiyofikika ambayo kwa asilimia kubwa yapo vijijini.
Ujinga mtupu
Kuna kodi kibao kwenye mafuta
 
Serikali ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuendelea kuiunganisha nchi kwa kutengeneza miundombinu mipya ya barabara katika maeneo yasiyofikika ambayo kwa asilimia kubwa yapo vijijini.
Naomba kujulishwa, ipo faida kuunganisha nchi kwa barabara na hata zile za angani,je sii hasara said kuitenganisha/kuigawanya nchi kwa itikadi za kisiasa, na kiuchumi na kutoyasikiliza matakwa ya wengi ,ikiwa ni pamoja na Kariba mpya iliyobeba mengi yanayohitaji marekebisho ya kweli,uhuru wa habari, uhuru wa maoni, uhuru wa kisheria kulinganga na matakwa ya katiba.
 
Nchi zote majirani zetu mafuta bei ipo chini na yanasafirishwa kwa malori kutokea Bandari yetu.Sisi tunashindwa wapi.? Wa mipakani angalau wao Wana nafuu shopping zao ufanyia nchi jirani hata fully tank ujazia kwa jirani. Kulewa wanalewea kwa jirani.
 
Ujinga mtupu
Kuna kodi kibao kwenye mafuta

IMG-20210711-WA0026.jpg
 
Solidarity fund na majizi, wahuni na mafisadi!?
Kwanza solidarity ipi bila consent ya mtoaji ? Waseme tu wanatuchangisha kurudisha pesa zao walizokosa kipindi cha aliyeenda
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Nalipwa basic salary 980K, baada ya makato yao lukuki naondoka na kama 510K.

Lakini wameona haitoshi, wanaendelea kuinyemelea tena hii 510K?

Naomba niwahakikishie viongozi wetu kwamba hata kama ningekuwa mzalendo kiasi gani saivi sina hata chembe ya huo uzalendo.

Na nikipata upenyo wa kupiga nitapiga mpaka senti ya mwisho.
 
Mswahili mwenye akili ni yule mwenye njaa
Kabisa mzee yani kabisa mwenye njaa ndio anaelewa au aliye nje ya madaraka! Nimeskiliza clip moja ya werema aliekuwa mwanasheria wa serikali! Anadai katiba mpya ni muhimu sababu madaraka ya raisi ni makubwa hatukatai ila mbona hajasema hilo akiwa mwanasheria mkuu wa serikali!
 
Hizo fedha zetu tunaomba zitumike kwa uwazi ... tupewe updates ya kiasi kinachopatikana na kinakwokwenda msije mkatumia kuhongea malaya DODOMA
 
Nalipwa basic salary 980K, baada ya makato yao lukuki naondoka na kama 510K.

Lakini wameona haitoshi, wanaendelea kuinyemelea tena hii 510K?

Naomba niwahakikishie viongozi wetu kwamba hata kama ningekuwa mzalendo kiasi gani saivi sina hata chembe ya huo uzalendo.

Na nikipata upenyo wa kupiga nitapiga mpaka senti ya mwisho.
Kabisa MKUU
 
Back
Top Bottom