Kuna siku nilisikia huyu mama anasema alisoma uchumi, mpaka unashangaa pamoja na taaluma yake hiyo ameshindwa kutambua kuwa kuongeza kodi ya dhuruma kwenye miamala ya simu ni kuuwa uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Serikali na wachumi uchwara wanakaa wanaweka jumla yakodi tatu kwenye muamala mmoja wa simu hizi si dharau za waziwazi nakutuona mazuzu ,wanapandisha kwa makusudi bei ya mafuta kitu ambacho ni kichocheo namba moja cha ushughuli za kiuchumi nchini.
Jambo la kuchekesha zaidi nikaona hapa hakuna kiongozi nikupunguza kodi kwenye vitu ambavyo havina tija kwenye uchumi wa nchii, yaani mtu anapunguza kodi kwenye betting/gambling ,pombe halafu anapandisha tozo kwenye gharama ya mafuta.
Yaani mama katika vipaumbele vyako vyote kwenye shughuli za kiuchumi nikuchochea kamali na unywaji pombe, vingine vyoote umepiga chini. Watu wanasema mwigulu anakufanyia hujuma sio kweli vitu vidogo kama hivyo havihitaji mpaka usome macro economics yaani umepwaya kweli kweli.
Oky kodi mmeshaanza kuchukua jee zitasaidia vipi wananchii kama sio kuibia masikini, Mama ebu rejea bajeti ya ofisi ya waziri mkuu ya mwaka 21/22 asilimia 80 ya bajeti yote ni matumizi binafsi asilima 20 ndio inapelekwa kwenye shughuli za maendelea.
Matumizi binafsi wanalipana posho mara mbili mbili, vikao visivyo na tija, wanakula bata huku wakiaacha raia kwenye janga la umasikini.
Uongozi mbovu,, muundo wa serikali mbovu, bunge bovu, katiba mbovu
Sent using
Jamii Forums mobile app
View attachment 1855593