Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 18,653
- 31,010
Natazama hapa Waziri Mwigulu Nchemba akiwa na maongezi na Wafaransa, ati kujenga viwanda vya madawa.
Kwanza, Kuna kiwanda cha madawa ya kukuua vidudu vya mbu Kibaha. Kiwanda hiki kimejengwa kwa ushirikiano na nchi ya Cuba.
Kiwanda vile vile kinazalisha dawa za binadamu.
Serikali yenyewe inakunyanyapaa na dawa zake hazinunuliwi na serikali yemyewe.
Pili , wafaransa ni nchi ya ukoloni mkongwe na wamefukuzwa Bukina Faso na Capt Ibrahim Traore. Ufaransa ina historia ya unyonyaji wa kupindukia.
Sasa Mwigulu and co. mnakumbatia mashetani hawa.
Viongozi wetu mnasukumwa na nini kushirikiana na hao mashetani, na mtakua lini kiakili?