Black Legend
Senior Member
- Jul 28, 2015
- 174
- 301
Ni habari ya kuhuzunisha kwa watumishi wa umma nchini, kupitia hotuba yake ya kusaini mikataba ya ujenzi wa reli ya mwendo kasi (SGR), Rais Samia Suluhu Hassan akitoa ufafanuzi wa ulipaji wa madeni alisema nchi lazima ilipe madeni ya nje kwasababu yame "Mature", akasisitiza kuwa tukikopa kama nchi basi ni vizuri na lazima kulipa.
Kwa kuendana na scenario hiyo, imekuwa ni huzuni kwa watumishi wa umma waliyowengi wenye madai ya malimbikizo ya mishahara na madai mengineyo kutosikia kauli ya mkuu wa nchi kuonesha kuwa serikali pia italipa madeni ya ndani yakiwepo madai ya watumishi.
Watumishi wamekuwa na kilio hiki cha muda mrefu lakini kasi na nia thabiti ya serikali ya ulipaji madai haya umekuwa ni mdogo mno.
Watumishi hawa ndiyo walipaji wakubwa wa kodi za serikali, watumishi hawa ndiyo ambao ni muda mrefu hawajaongezewa mishahara ilhali gharama za maisha zinapanda kila kukicha, lakini mbaya zaidi hata kile wanachodai hawalipwi.
Tanzania ni yetu sote, kama tumeshindwa kuwapa mazingira bora ya ufanyaji na utendaji kazi basi ifike muda watumishi walipwe kile wanachoidai serikali. Nasisitiza tena na tena "Tanzania ni yetu sote".