Wana Mwenge Jazz Paselepa waliimba, wewe ukisema mke gani we bwana wenzio wanamuona anapeendeza. Hamuoni umuhimu wa hivi vituo SI mpo mjini huduma tele mnabeza tu. Huko vijijini ni faraja kubwa Sana, wananchi wanateseka Sana kwenye hizi huduma muhimu. Mimi nilikuwa kati ya watu tuliombeza Sana Mh. Kikwete, lkn Kuna siku nilipata mgonjwa wa Sukari, alikuwa na hali mbaya Sana, na mjuavyo watu wazima wengi akiwa na Sukari lzm awe na pressure. Tulihangaika Sana Hindu Mandal bila suluhisho. Tulishauriwa tuende Muhimbili, hakuna aliyekuwa na hope na Muhimbili maana wakati ule private zilikuwa na sifa zote.
Muhimbili tulifanikiwa kupata clinic Safi Sana ya Moyo chini ya Dr. Kissenge, alitupa program nzuri Sana ingawa yeye SI dokta wa Sukari lkn aliweza kufanya mgonjwa wetu apate nafuu na Sukari yake ikashuka Sana, akawa Yuko normal. Sasa nikawa nikiona like jengo pale JAKAYA KIKWETE roho inanisuta nabakia kusema mnyonge mnyongeni haki yake mpe.
Mwendokasi nao ile barabara wakati inajengwa duh kelele hapa JF watu wanabeza kila mtu na utaalam wake, lkn hayooo yanapiga kazi though Kuna mapugufu kwenye uendeshaji lkn miundombinu ipo.
Kelele tena zipo kwenye hizi projects kubwa km umeme wa Mwalimu Nyerere kule rufiji watu wanaandika kabsaa hizo ni white elephant projects lakini siku zinakwenda miradi inaelekea ukingoni. Sgr nayo hiyooo! Inachanjq mbuga.
Juzi nimeona kwenye Facebook page ya mheshimiwa Eng. Manyaya kaweka muonekano mpya wa mji wa Mbambabay kule Nyansa, Kwanza full lami, usiku taa zinawaka yaani mji uko byee kabisa. Kwa wale wanaotoka pande hizo waulize Mambo yalikuwaje kabla na Sasa. Sehemu ya kwenda masaa matano unatembea siku mbili. All in all usiibeze serikali hasa inapojenga kule kwenu halafu wewe huna habari nako, hata kibanda Cha kuku hujajenga, tunajiona wa mjini Sana! Wakati wazee wetu wapo huko vijijini wanapata tabu.
Nnachowasihi furahieni hata serikali inawakumbuka kwa maendeleo otherwise nchi inaweza kuwa km Congo au Guinea kila siku mnanyang'anyana madaraka na wajeda!