Hao washirika wa maendeleo waliwaambia watatoa hicho kiasi, au ni wishful thinking ya Mwigulu na Samia?
Kama wasipotoa tunarudi kule kwenye nakisi ya bajeti, matokeo yake pesa hazitafika mawizarani kama ambavyo wizara husika ziliomba..
Baada ya hapo ni mkwamo, miradi kadhaa haitasogea, licha ya serikali hiyo hiyo kuwa tayari ilishakopa trilioni kadhaa kwa ajili ya kuongezea kwenye bajeti hiyo hiyo..
Umaskini ni mbaya asikwambie mtu, unaweza kuwa na shida ya kiasi fulani cha pesa, ukaomba ukaomba lakini bado usipate kile ulichohitaji, bado ukaamua na kukopa kabisa, lakini bado kuna baadhi ya mambo yako hayatasogea!.
Lakini ajabu ya karne sasa, utakuta viongozi hao hao wanaoshuhudia huo mkwamo, bado wanatoa pesa nyingi kwaajili ya kununua v8 zenye viyoyozi ili ziwape raha wakiwa safarini, hapa ndipo utatambua kama taifa tu maskini wa akili pia.