Waziri Mwigulu: Tunatazamia kuwakopesha Wafanyakazi wenye sifa Magari ili kupunguza Matumizi ya Serikali

Halafu hawa wakuu wa wilaya walio mijini. Wakurugenzi, wakuu wa miko V8 za nini,
Na miundombinu hipo sawa.
Toyota land cruiser mkonga irudi mzigoni.

V8 iliingia Awamu ya 4 Kwa sifa tu za viongozi kupendanufahari wa mchongo.
 
Awamu ya sita ikimaliza utawala wake nchi itakuwa imefilisika na hakutakuwa na maisha daraja ya kati ila ni matajiri saana maana ya wafanyakazibiashara na mafukara wa kutupwa!
Ifikisike Kwa lipi? Kuna awamu inazalisha pesa nyingi kupita awamu ya 6?
 
Toyota land cruiser mkonga irudi mzigoni.

V8 iliingia Awamu ya 4 Kwa sifa tu za viongozi kupendanufahari wa mchongo.
Tatizo jamaa wana 10% kwenye huo mkataba wa toyota, so kila siku zitakuwa ngonjera tuu, kuna watu wanaonufaika sana na huo mkataba.
 
Hapo kwenye public transport Bado Kuna hatua kadhaa Ili kupafikia.

Mkwamo wa kiuchumi unakuja ndo unawalazimisha kuchukua hatua hizo.

Tukiondokana na V8 Kwa DC,RC, KATIBU WAKUU NA WASAIDIZI MAWIZARANI, wakakopeshwa Toyota land cruiser mkonga, mbona itapunguza Mzigo Kwa wananchi!!
 
Tatizo jamaa wana 10% kwenye huo mkataba wa toyota, so kila siku zitakuwa ngonjera tuu, kuna watu wanaonufaika sana na huo mkataba.
Ni sawa, watalazimika kuvunja mkataba huo,

Ukimsikia mwigu, Serikali imepanga kukopa Ili kulipa riba na mikopo budget ijayo.

Hali ni Tete, yajayo Si mazuri.
 
Kitakachofanyika ni kuvujisha kapu la serikali na kutumia fedha ya serikali hiyohiyo kujilipia huo mkopo
 
Hili zoezi lilishawahi kufanyika kabla hawajauziana nyumba za Serikali na likafeli

Uzalendo wa Wanyarwanda siyo wa kutanguliza Tumbo tofauti na hapa kwetu Watu Wana matumbo ya tembo
Unakopeshwa mwenyewe na unapimiwa mafuta Sasa Ukiharibu Utajua mwenyewe ila we want our kazi be done.

Sijaelewa Bado shida itakuwa ni wapi? Mbona Kwa wabunge lomewezekana?
 
Watasingizia fedha za maintenance n.k
 
Hili gumu DED akihamishwa mnanunua gari lingine la kumkopesha DED mpya?
Hizi gharama za kukarabati si ni nyie mlio ziendekeza kwa kuvunja karakana halmashauri ?
Kwani kwa wabunge wabafanyaje, mbona mambo uenda vizuri
 
Your browser is not able to display this video.
Akijibu swali la Mbunge Asia Abdulkarim Halamga aliyehoji sababu za Serikali kutumia Wakala wa Huduma za Ununuzi Serikalini (GPSA) ambaye ananunua Magari kwa gharama kubwa kuliko bei ya Soko la Dunia, Waziri wa Fedha, Dkt, Mwigulu Nchemba amesema Serikali inatazamia kuanza kuwakopesha Watumishi wenye sifa ili kuondoa mzigo wa Mafuta na Matengenezo Serikalini.

Kuhusu utaratibu wa kuagiza Magari moja kwa moja Viwandani badala ya kutumia Mawakala, Dkt. Mwigulu amesema "Kuna baadhi ya mazingira yanaruhusu Serikali kununua kwa mawakala, pia, baadhi ya Viwanda havipendi wanunuzi waende moja kwa moja Viwandani".

Kwa mujibu wa taarifa iliyowasilishwa na Wizara ya Fedha Bungeni mwaka 2022, Serikali ilikuwa na Magari 15,742, Pikipiki 14,047 na Mitambo 373 huku ikitumia zaidi ya Tsh. Bilioni 500 kila mwaka kwaajili ya Ununuzi wa Magari mapya, Mafuta, Vipuri na Matengenezo.
 

Deal jingine linazaliwa upya. Halafu baadae tutamwita CAG. Halafu tutajadili bungeni. Halafu tutaishia kulalamika.

Kuna wakati hakuna sababu ya kukasirika maana mchimba kaburi, lazima atumbukie mwenyewe kwanza. Yangu macho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…