Waziri Mwigulu: Tunatazamia kuwakopesha Wafanyakazi wenye sifa Magari ili kupunguza Matumizi ya Serikali

Waziri Mwigulu: Tunatazamia kuwakopesha Wafanyakazi wenye sifa Magari ili kupunguza Matumizi ya Serikali

Madereva hawatoguswa,

Mav8 ndo yatayeyuka.
Ok......Sasa mtu akopeshwe gari, service apeleke mwenyewe, mafuta ajaze mwenyewe halafu akubali liendeshwe na mtu mwingine? Ambaye huenda ana uendeshaji mbaya itakayompelekea bosi kwenda gereji kila mara kwa pesa zake? Difficult.
 
idea nzuri ila sasa huwezi mkopesha mtu gari la mil 300... labda kama wataanza kutembelea vanduard hiyo ndo top top the rest vitz.
 
Serikali iliwahi kusema inatumia Bil.550 Kwa mwaka Kuagiza magari, vipuri, mafuta na matengenezo Kila mwaka.

--
“Mtazamo wa Serikali ni kuendelea kupunguza masuala ya matumizi ya magari [...] Badala ya serikali kuwa inamiliki haya magari, tunataka watumishi wanaopata sifa ya kuwa na magari wakopeshwe yawe ya kwao ili kuipunguzia Serikali mzigo wa kuyaendesha magari, kuyapatia ‘service’ pamoja na vitu vingine vinavyotakiwa.” – Dkt. Mwigulu Nchemba


View: https://twitter.com/swahilitimes/status/1722154691599925379?t=UwMJqonggWDnKfg-JyS9WA&s=19

My Take
Naona Kuna kigugumizi Cha kuchukua maamuzi.

Toka mwaka juzi mnaongelea hili jambo na hamfiki Muafaka.

Semeni kama Serikali kwamba deadline itakuwa lini? Na Je Madereva mtaajiri wa Umma au Kila boss na dereva wake?

Kitakachofanyika ni kuvujisha kapu la serikali na kutumia fedha ya serikali hiyohiyo kujilipia huo mkopo
 
Mimi naona kama meli inazama tu, nahodha ni kama hatuna vile. Au wenye vigezo watakopeshwa vanguard, Harrier na wanaofanana na hao? Manake vx v8 ukimkopesha mtu anayepata 4m atalipa lini amalize.
 
Ok......Sasa mtu akopeshwe gari, service apeleke mwenyewe, mafuta ajaze mwenyewe halafu akubali liendeshwe na mtu mwingine? Ambaye huenda ana uendeshaji mbaya itakayompelekea bosi kwenda gereji kila mara kwa pesa zake? Difficult.
ni idea ambayo haiwezi kufanya kazi kama wameona mzigo mkubwa wapunguze idadi ya watumishi wanaostahilii magari ya serikali
 
Yaani ukopeshe mtu gari ya 600mil 😃
Hatari sana. Sema mambo yenyewe ya vificho ficho. Wanatakiwa waonyeshe mpango kazi. Watumishi gani watawakopesha? Magari aina gani? Mtu akiachishwa majukumu yake mkopo utakuwa na hali gani? Je hakuna option nyingine zaidi ya hiyo ya kukopeshana??
 
Back
Top Bottom